Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Godwin Gondwe ametoa siku 14 kwa Mzabuni wa vifaa tiba Bahari Phamacy kuhakikisha vifaa hivyo vinapatikana ndani ya siku kumi na nne kuanzia leo.
Sambamba na hilo amemtaka mzabuni wa samani katika Hospitali hiyo ambaye ni "Jaffery Industries" hadi kufikia tarehe 16/03/2021 awe ameweka Samani zote kwa mujibu wa mkataba katika kituo hicho cha Afya.
Ametoa maagizo hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya Kituo hicho cha Afya cha kisasa, mradi unaotekelezwa na Mradi wa uboreshaji wa jiji la Dar es salaam(DMDP).
Akiwa katika kituo hicho cha Afya alipata wasaa wa kukikagua na kupata taarifa ya gharama ya ujenzi wa kituo hicho ambapo hadi kukamilika kwake itagharimu Bilioni 4.4 ambapo bilioni 2.2 ni ujenzi wa jengo na 2.2 vifaa tiba na samani,kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mganga Mkuu wa Manispaa Dkt Gwamaka Mwabulambo.
"Wananchi wa Buza wanataka kuona kituo cha Afya kinafanya kazi hivyo lazima kazi zifanyike kwa kuzingatia mkataba na kazi zikamilike kwa wakati" Alisema Mhe Gondwe.
Ifahamike kuwa Kata ya Buza pekee ina miradi yenye thamani zaidi ya bilioni 18 ambayo inatekelezwa na DMDP ambayo ni Kituo cha Afya pamoja na miradi mingine ya barabara.
Aidha katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya aliambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama, Katibu Tawala wa Wilaya pamoja na wataalamu kutoka Manispaa.
Mhe. Mkuu wa Wilaya ameonyesha kuridhishwa na ujenzi wa jengo la kituo cha afya Buza na kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo.
Baadhi ya matukio katika picha yakionyesha Mhe .Mkuu wa wilaya wakati wa ukaguzi wa kituo cha afya Buza Temeke Jijini Dar es Salaam.
Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.
Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam
Simu ya Mezani: +255 22-2928132
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz
Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke