Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh; Felix Lyaniva azindua jukwaa la wanawake kiwilaya katika viwanja vya Mwembe Yanga. Katika uzinduzi huo DC Lyaniva asisitiza wanawake kupendana, kuwa na umoja ili kujiletea maendeleo ya kweli,hata kufikia uchumi wa kati.
Katika uzinduzi huo ulifanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Kiwilaya ambapo Johari Maulid Mkonde alichaguliwa rasmi.
Jukwaa la wanawake liliundwa ili kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuondoa pengo kubwa ambalo limejengeka duniani na kuongeza ushiriki wa wanawake katika uchumi duniani kote.
Kauli mbiu katika uzinduzi huu nI ''Mwanamke Tumia Fursa Kushiriki Uchumi wa Viwanda''
Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.
Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam
Simu ya Mezani: +255 22-2928132
Simu ya Mkononi: +255 755 415 152
Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz
Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke