• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

BILIONI 261 KUTUMIKA UJENZI WA MIUNDO MBINU YA MWENDO KASI

Posted on: November 26th, 2020

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Godwin Gondwe amefanya ziara kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka (BRT) barabara ya Kilwa ( Kilwa Road).

Ziara hiyo imefanyika jana mchana ambapo Mhe. Gondwe akiwa na timu ya wataalamu kutoka taasisi mbalimbali wilayani humo, ametembelea eneo linalojengwa 'flyovers' vituo vya kupakia na kushusha abiria (Vituo mlisho 'feeder stations'),barabara, pamoja na kituo kikuu (Terminal) cha BRT Mbagala Rangi Tatu ambacho kinajumuisha vituo mlisho 6,karakana,sehemu ya maegesho ya mabasi yaendayo haraka,sehemu ya maegesho ya mabasi ya abiria (daladala), sehemu ya kujaza magari mafuta,na sehemu ya maegesho ya magari binafsi.

Akizungumza wakati akihitimisha ziara yake  Mhe. Gondwe amesema" kwanza nianze kwa kumshukuru Mhe Rais kwa kutuletea mradi mkubwa Temeke,mradi huu gharama yake ni sh.bilioni 261,nataka nichukue fursa hii kuwaambia Wana Temeke kwamba Dkt. John Pombe Magufuli yupo kwa ajili yao,na anaendelea kuboresha miundombinu ili wao waweze kusafiri vizuri"

Aidha  amewataka waliopewa kusimamia ,pamoja na wanaofanya kazi ya ujenzi,kufanya kazi vizuri na kwa wakati" Na ninyi mnaofanya kazi hii,Serikali imewaamini,TANROADS ninyi ndio waajiri,simamieni kazi vizuri.Mhandisi mshauri afanye kazi yake inavyotakiwa,na wale ambao ni wajenzi wahakikishe kwamba wanafanya kazi ndani muda wa mkataba ambao wamekubaliana na Serikali ili mradi huu usichukue muda mrefu kukamilika,wananchi waweze kunufaika mapema na miundo mbinu mikubwa ambayo inatengenezwa . 

"Amesisitiza Mhe.Gondwe.Vilevile Mhe. Gondwe amewataka TANROADS  kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa mkataba,endapo  kazi hiyo haitakamilika ndani ya muda wa makubaliano.Katika hatua nyingine Mhe. Gondwe ameagiza kushughulikiwa kwa haraka changamoto zote zinazosababisha mradi huo kutokwenda kwa kasi iliyokusudiwa.Kazi za ujenzi wa Mradi  wa miundo mbinu ya BRT zimegawanywa katika sehemu 2 (LOTS),ambapo LOT 1  inahusisha  ujenzi wa barabara ( KM 20.3),'Flyovers' 2,vituo vya  mabasi 29 na daraja moja la juu la waenda kwa miguu.LOT 2 inahusisha  ujenzi wa karakana ( Depot),vituo vikuu na vituo Mlisho 4.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke