• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

DC JOKATE AENDELEA KUTATUA KERO YA MAJI MASHULENI.

Posted on: February 17th, 2022

TUTAENDELEA KUTATUA KERO YA MAJI MASHULENI - DC TEMEKE

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Jokate Mwegelo amesema changamoto za upatikanaji wa matundu ya vyoo, maji safi na salama katika shule za sekondari zitaendelea kutatuliwa ili kuwanufaisha wanafunzi na walimu wilayani Temeke.

Ameyasema hayo siku ya Februari 10, 2022 katika hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa visima viwili vya maji iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Mbagala iliyopo kata ya Mbagala kuu pamoja na Dovya iliyopo kata ya Chamazi Wilaya ya Temeke.

Aidha Mhe. Jokate amemshukuru mwakilishi kutoka shirika la Hayrat Yardim Ndugu Yusuf Kara ambao wamefadhili uchimbaji na ujenzi wa visima hivyo huku akiendelea kuwaomba kutokuishia hapo na kuwataka waendelee kusaidia shule nyingine ili kuimarisha miundombinu ya elimu kwa kumuunga mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa vitendo.

"Lazima miundombinu yetu yote iendane na uchumi wa hadhi ya mkoa wetu, wilaya yetu na kata zetu naamini tukiendelea kuweka jitihada  mahsusi tutafanikiwa na watoto wetu watakuwa na mazingira bora ya kujifunza, lakini pia walimu wetu watakuwa na mazingira mazuri ya kuwafundisha wanafunzi wetu". Alisema Mhe. Jokate

Pia katika kuhakikisha anaongeza ufaulu wilaya ya Temeke Mhe. Jokate amesema wamejipanga kuunda kamati maalumu kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Elimu Dar es salaam (DUCE) ili kusaidiana katika kukabiliana na changamoto za elimu pamoja na kuongeza uwezo wa walimu kufundisha vizuri.

Naye mwakilishi kutoka Uturuki wa Shirika la Hayrat Yardim Ndugu Yusuf amesema anaamini mchango huu wa visima utasaidia kurahisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wanafunzi wa shule hizo huku akiahidi kuchangia viti na meza 50 shule ya Sekondari Mbagala na kuendelea kujenga visima vingine ili kuisaidia jamii kutatua kero ya maji.

Sambamba na hayo Mhe. Jokate ameipongeza Shule ya Sekondari Mbagala kwa kufanya vizuri matokeo ya kidato cha 2 na 4 wilayani humo huku akiendelea kuhimiza walimu, jamii, viongozi na wadau mbalimbali wa maendeleo kushirikiana kuijenga jamii iliyobora kupitia elimu katika mazingira mazuri.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke