• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

DC JOKATE AWATANGAZIA NEEMAWAKAZI WA CHAMAZI

Posted on: June 25th, 2022

Na Sweetbetter Njige TMC Habari.

Juni 24,2022 mkuu wa wilaya ya Temeke mheshimiwa Jokate Mwegelo amefanya ziara  katika kata ya Chamazi, mtaa wa Mbande Magengeni, kwa lengo la kusikiliza kero za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Katika ziara hiyo Mhe. Jokate aliambatana na mkurugenzi wa manispaa ndugu Elihuruma Mabelya, diwani wa kata ya Chamazi  Mhe. John Laurent Gama, wakuu wa idara za manispaa ya Temeke na wakuu wa  taasisi mbalimbali za Umma wakiwemo wa  TANESCO,NSSF, Jeshi la Uhamiaji na TARURA   ambapo Wananchi walipata wasaa wa kueleza kero zao na kupata majibu ya kero hizo moja kwa moja.

Wakati wa hotuba yake Mhe. Jokate aliwashukuru Wananchi kwa kujitokeza kwa wingi na kutoa kero zao, njia ambayo itasaidia kuboresha hali ya mazingira ya upatikanaji na utoaji huduma.

"Changamoto hazikosekani kwenye njia ya kuyafikia maendeleo, nampongeza Mhe. Diwani kwa maendeleo anayopata katika kata, shule mpya yenye jumla ya vyumba 20 imejengwa kwa nguvu za Rais wetu Samia Suluhu Hassan.

Kupitia ruzuku na mapato ya ndani Mkurugenzi amefanikiwa kutoa milioni 470 kwa ajili ya  ujenzi wa shule ya msingi Dovya  kupunguza mzigo kwenye shule nyingine, na kituo chetu cha polisi kinaenda kumalizika hivyo tutaimarisha ulinzi,tunatarajia miradi mingi zaidi katika kata hii kama vile kituo cha afya mtaa wa Mkondogwa kinachojengwa kwa milioni 500,TARURA wana mpango wa kujenga barabara za mitaa kwenye kata hii,hivyo tutafanikiwa kupunguza ama kuondoa kabisa kero zilizosemwa hapa kwa kiasi kikubwa"

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi  Mhe. Gama ametoa shukrani za dhati na kumpongeza Mhe. Jokate kwa kuamua kuwafikia kujua hali halisi ya changamoto na kero za Wananchi na kuzitolea ufumbuzi.

Kwa upande wake mkurugenzi Mabelya amesema kwamba

Manispaa imejipanga ipasavyo kuwahudumia Wananchi, na kwamba wasiwe na hofu kwani katika mwaka wa fedha ujao (2022/2023) wamejipanga kuboresha na kukarabati masoko na huduma nyingine mbalimbali ili wakusanye mapato huku Wananchi wakifurahia huduma.

 Aidha ametoa wito kwa Watendaji kutoa huduma katika namna bora ili kupunguza kero ndogo ndogo kwa Wananchi.

Ziara hiyo ya Mhe. Jokate ni muendelezo wa ziara zake ambazo amekuwa akizifanya katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Temeke. Kupitia ziara hizo kero nyingi zimepatiwa ufumbuzi .

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke