• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

DC JOKETI AAMURU VIONGOZI WA CHUO KUWEKWA CHINI YA ULINZI

Posted on: September 1st, 2021


Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Urban Mwegelo leo Agosti 31,2021 ameungana na wataalam katika ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Akiwa ameambatana na Mkurugenzi-Uthibiti,Ufuatiliaji na Tathmini kutoka NACTE Dkt. Joefrey Oleke walibaini uwepo wa chuo kinachoendeshwa kinyume cha sheria kinachojulikana kama LUBANGO TRAINING COLLEGE kilichopo katika kata ya Mtoni Kijichi mtaa wa Butiama.

Baada ya kufanya mahojiano na mkuu wa chuo,Mhe. Mwegelo aligundua kuwa kwa muda sasa chuo hicho kimekua kikitoa mafunzo bila kupata usajili, pamoja na kutoa mafunzo kwenye mazingira yasiyo rasmi .

"Hamna kitu kibaya kama kufanya utapeli halafu ukadhani hutagundulika,Serikali ina macho kila sehemu,NACTE kaeni hapa na jeshi la Polisi, lazima tupate 'information',chuo hakijasajiliwa lakini hata mandhari yake haistahili,kuna watu wanatoa huduma ambazo kiuhalisia hawastahili kutoa, tushirikiane katika ufuatiliaji, hawa wachukuliwe hatua kali huu ni utapeli" Alisema mkuu huyo wa wilaya.

Kwa upande wake Dkt. Jofrey Oleke amesitisha shughuli zote zinazoendelea katika chuo hicho,huku akielekeza taratibu nyingine za kisheria kufuata.

Aidha Dkt. Oleke amesema kuwa kwa ukaguzi uliofanyika, chuo hicho hakitambuliki NACTE wala VETA.

"Hiki sio chuo ambacho kimesajiliwa na kina'operate' kinyume na taratibu za Nchi, na sisi kama baraza tunasitisha shughuli zote za training katika sehemu hii mpaka pale kitakapokua kimesajiliwa. Lakini pia tutoe rai kwa Wananchi,wasikubali kuleta watoto wao katika vyuo vya uchochoroni, na kama kuna vyuo kama hivi watuambie ili kudhibiti" alisisitiza Dkt. Oleke.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Mwegelo ameamuru viongozi wa chuo hicho kuwa chini ya ulinzi na wanafunzi waliokutwa chuoni hapo kuchukuliwa maelezo ikiwemo mkuu wa chuo hicho Ndg. Geofrey Njegero Mtembeli.

Katika hatua nyingine Mhe. Mwegelo ametembelea miradi ya masoko,miradi ya kufyatua matofali inayoendeshwa na vijana kwa kutumia mikopo iliyotokana na 10% ya mapato ya ndani ya halmashauri ya manispaa ya Temeke, ikiwemo viwanda vya kufyatua matofali vya Toangoma na Ruvuma.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke