• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

DC Temeke Akutana na Wadau wa Elimu

Posted on: April 19th, 2021

Baadhi ya walimu wakifuatilia kikao kazi ndani ya ukumbi wa Manispaa kilichoandaliwa na mkuu wa Wilaya.

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Godwin Gondwe amefanya kikao kazi na wadau wa ndanbi wa elimu.

Kikao hicho chenye lengo la kukuza ufaulu katika wilaya ya Temeke kimefanyika leo mchana,katika ukumbi wa Manispaa( Iddi Nyundo).

Katika kikao hicho kilichowahusisha Wakuu wa idara za Elimu Msingi na Sekondari,Maafisa Elimu,Waratibu Elimu Kata,Wadhibiti Ubora wa Shule, Watendaji wa Kata, Wakuu wa shule za Sekondari na walimu wakuu wa Shule za Msingi wote,Mhe. Gondwe amesema kwamba lengo la kikao hicho ni kuwakutanisha pamoja wadau wote wa elimu wa ndani,ili kupeana uzoefu,kujadili kwa pamoja kuhusu elimu.Kusikiliza changamoto za walimu,pamoja na kujadili kuhusu  namna bora ya kuinua kiwango cha ufaulu.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho Mhe. Gondwe amewataka wadau wote wa elimu  wa ndani kuifanya elimu kuwa ajenda yao ya kila siku."Ajenda ya elimu iwe ni ajenda endelevu.Mkitoka hapa mkawaambie viongozi wenzenu kule kwenye kata kwamba kila mkikaa elimu iwe ni ajenda yenu.Amesisitiza Mhe. Gondwe.

Aidha Mhe. Gondwe ametoa maelekezo kwamba makubaliano yote  ambayo wamekubaliana katika kikao hicho ,yawekwe kwenye nyaraka moja kama mikakati ya pamoja ya kuongeza ufaulu.

Kadhalika ameelekeza kufanyika kwa makubaliano kati ya Mkurugenzi,watendaji wa kata na maafisa elimu,makubaliano kati ya maafisa elimu na waratibu elimu kata,Waratibu Elimu Kata  na walimu Wakuu pamoja na  Wakuu wa Shule.Walimu Wakuu/ Wakuu wa Shule na Walimu wao.Amesema kwamba kwa kufanya hivyo,itasaidia kila mmoja kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Katika hatua nyingine Mhe. Gondwe amewapongeza walimu wote wa Temeke kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuhakikisha kwamba wanatoa matokeo mazuri kwa watahiniwa wao,pamoja na changamoto  ya kuwepo kwa wanafunzi wengi mashuleni,na changamoto kadhaa zinazohusu maslahi yao.

Kwa upande wao wadau wa ndani wa elimu  ambao walipata fursa ya kuzungumza kuhusiana na kikao hicho,wamemshukuru sana Mhe. Gondwe kwa kuitisha kikao hicho,ambapo wamesema kwamba ni mara ya kwanza kwa wao kukaa pamoja na Mhe .DC kujadili kuhusu elimu,na kwamba kikao hicho kimekuwa cha manufaa makubwa ,kimewabadilisha sana mitazamo,na hawana shaka kwamba kiwango cha ufaulu kitakuwa cha hali ya juu.

Mhe. Gondwe amekuwa akifanya vikao mbalimbali vya wadau  wilayani Temeke.Kikao hicho cha wadau wa elimu ni muendelezo wa vikao vyake vingi ambayo amekuwa akivifanya kwa lengo la kuboresha mahusiano na kuipeleka mbele Temeke.Hata hivyo kikao hicho kama ilivyokuwa kwa vikao kadhaa vilivyopita kimekuwa cha kihistoria,na kuweka alama kubwa katika mioyo na fikra za walimu,na wadau wote wa ndani wa elimu kwa ujumla

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke