• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

DOKTA SAMIA AMEJIPANGA KUTENGENEZA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAZALISHAJI- WAZIRI JAFFO

Posted on: October 3rd, 2024

Na: Sweetbetter Njige

       TMC Habari.


Leo Oktoba 2, 2024 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Sulemani S. Jaffo ameongoza hafla fupi ya kufunga Maonesho ya Kimataifa ya Viwanda (TIMEXPO) yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere (Sabasaba) Temeke, Dar es Salaam.


Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Jaffo amesema ni fahari kwa Watanzania kuzalisha, kusambaza na kutumia bidhaa zilizozalishwa ndani ya Nchi na kuwa Serikali imejipanga kuboresha mazingira kwa wazalishaji ili kuimarisha biashara na ajira. Amesema


"Watanzania tuamke, tujivunie vya kwetu, nimeona fahari sana kukagua bidhaa na zimeandikwa 'made in Tanzania'...Serikali ya Rais Samia inaendelea kutengeneza mazingira wezeshi kuhakikisha uwekezaji wa viwanda na uchumi unaenda vizuri. Sisi kama watendaji, tutajitahidi kupitia mambo yenye kuleta changamoto kubwa yanatatuliwa ili kuhakikisha bidhaa za ndani zinapata masoko kwa ajili ya kutunza ajira na uendelevu wa viwanda hivi"


Aidha Mhe. Jaffo amewapongeza wazalishaji wote ikiwemo wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuzalisha ajira kwa vijana kama lilivyo lengo la sekta binafsi ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. 


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Temeke mhe. Sixtus Mapunda amesema


"Nawashukuru waandaji wa maonesho haya CTI (Confederation of Tanzania Industries) na Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (Tantrade) kwa maonesho mazuri, naamini Temeke tutaendelea kuwa wenyeji kwa maonesho haya ambayo naamini yatakuwa ya pili kwa ukubwa baada ya yale ya sabasaba".


Maonesho ya kimataifa ya viwanda yamefanyika mara ya pili na kwa mafanikio makubwa kutokaka kuwa na washiriki 79 mwaka 2023 kufikia washiriki 257 mwaka 2024.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke