• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yazidi kutanua wigo katika sekta Afya.

Posted on: June 10th, 2019

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wameendelea na kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii iCHF (improved Community Health Fund) lengo kuu likiwa ni kuhakikisha wakazi wa Wilaya ya Temeke hasa wenye kipato cha chini wanapata huduma ya  matibabu kwa urahisi.

 Kwa Wilaya ya Temeke Huduma kwa kadi  zinapatikana katika vituo vyote vya Serikali ambavyo ni Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali ya Wilaya pamoja na Hospitali ya Mkoa na mpaka sasa kwa Wilaya ya Temeke yenye kata 23 kuna zaidi ya wanachama 536 wanaohudumiwa na Bima hii.

Katika uhamasishaji huo wa kuhakikisha kila mwananchi wa Manispaa anapata elimu ya Afya, na kuelezwa faida za kujiunga na mfuko wa matibabu kupitia bima ya afya ambapo wameelezwa kuwa, gharama ya bima hiyo kwa mtu mmoja ni shilingi 40,000/- kwa mwaka na katika kaya yenye watu 6,  ambapo wakuu wa kaya 2 na watoto 4 wenye umri chini ya miaka 18 watakatwa kiasi cha shilingi 150,000/- kwa mwaka kama gharama za matibabu kwa kutumia bima hiyo.

Nae Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dr.Gwamaka Mwabulambo amesema, mwitikio wa wananchi wa Wilaya ya Temeke kuhusu kadi za matibabu ni wawastani, japo elimu inazidi kutolewa kwa kiasi kikubwa ili kupata wanachama wengi zaidi kwakuwa suala la afya ni la msingi zaidi kwa ustawi wa Manispaa na Taifa kwa  ujumla.

“Kazi kubwa ni kuhakikisha dawa zinapatikana na wanachama wetu wanapata huduma stahiki ,hivyo niwasihi wananchi kuhakikisha wanakata bima hii, kwa kuwa kuna wakati huna fedha hiyo ya matibabu lakini kwakuwa unabima basi una uhakika wa kupata matibabu kwa wakati” Alisema Dr.Mwabulambo.

Nae Mratibu wa Bima ya Afya ya iCHF wa Manispaa wa Temeke ndugu Christian Mwaisoloka Alisema, timu ya uratibu wa bima hiyo imejizatiti kuhakikisha elimu inawafikia wananchi wote ili kupata wanachama wa kutosha na kuhakikisha afya bora inapatikana kwa wakazi kwa maendeleo endelevu

“Mkakati tulio nao kwa sasa ni kupita na gari la matangazo ili kuwahabarisha umma faida za kuwa na bima hii  pamoja na kubandika matangazo maeneo mbalimbali pamoja na kuandaa mikutano ya hadhara kwaajili ya elimu ya Afya na umuhimu wa bima hiyo”.

Sambamba na kadi ya iCHF Manispaa ya Temeke imejizatiti kuhakikisha afya ya wakazi wake hususani wazee inaimarika kwani ilifanikiwa kutengeneza vitambulisho 10,576 vya Afya, vya  bure vya wazee kwaajili ya kurahisisha matibabu na kuboresha afya zao na inampango wa kutengeneza vitambulisho vingi zaidi katika awamu ijayo.Alisema Christian.

Kitambulisho cha huduma bure kwa wazee (Kadi) kinapatikana papo kwa hapo na huduma rasmi ya matibabu huanza kutolewa baada ya siku 14 na (matibabu) kwa kadi  hiyo ya wazee hutolewa ndani na nje ya Mkoa alipopatia kadi hiyo hivyo kuwatoa hofu wazee kuhusu matibabu ya afya zao popote watakapokuwa, alibainisha zaidi mratibu huyo.

Ikumbukwe kuwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ipo katika hatua ya kuhakikisha watu wote wanatumia bima ya Afya. Lengo ni kuondoa changamato zinazowakabili wananchi wengi na hasa wa vijijini pindi wanapokuwa na matatizo ya Kiafya.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke