• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

"Jitihada Hizi za Usafishaji na Utunzaji wa Mazingira Ziendelezwe" LEAT

Posted on: June 16th, 2021

Maafisa sheria kutoka LEAT,Maafisa kutoka Manispaa ya Temeke,Afisa mtendaji wa kata ya Mbagalakuu na Mwenyekiti wa mtaa wa Mbagalakuu Mashariki wakiwa katika ziara ,soko la Njia ya Ng'ombe,kukagua hali ya usafi na utunzaji  wa mazingira ya soko hilo.

Maafisa sheria kutoka LEAT,Maafisa kutoka Manispaa,Viongozi wa kata na mtaa wakiwa katika majumuisho,mara baada ya ziara ya ukaguzi wa hali ya usafi na utunzaji wa mazingira ya soko la Njia ya Ng'ombe.


Kauli hiyo imetolewa na Afisa sheria  kutoka  Shirika  la Lawyers' Environmental Action Team (LEAT) wakili Baraka Thomas mara baada ya ziara fupi iliyofanywa na Maafisa wa shirika hilo kwa kushirikiana na Maafisa Mazingira na Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka manispaa ya Temeke,pamoja na uongozi wa kata ya Mbagala kuu na serikali ya mtaa wa Mbagala kuu Mashariki,ambapo walitembelea katika soko la Njia ya Ngombe lililopo katika kata ya Mbagala kuu ,soko ambalo   siku za nyuma  lilionekana kuwa na changamoto kubwa ya uchafuzi wa mazingira.


Ziara hiyo iliyofanyika jana Jumatano, ililenga kuangalia hali  ya usafi wa mazingira katika eneo hilo .


Akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara hiyo, yaliyofanyika katika ofisi ya Mtendaji wa kata, wakili Thomas amesema "Leo katika ziara yetu tumetembelea soko la Njia ya ng'ombe, katika kata ya Mbagala Kuu,tukiwa sisi pamoja na watumishi wa Manispaa,lakini pia na viongozi wetu wa Kata na serikali ya Mtaa.


Tumeona kwamba kuna shughuli  za kibinadamu ambazo zinafanyika katika eneo hilo,lakini miundombinu ya usafi kwa mfano utiririshaji maji, baada ya watu kufanya shughuli zao za usafi,upishi na kadhalika ni changamoto, lakini tumeona pia kwamba kuna jitihada kubwa zimefanyika kutoka serikali ya mtaa,na kata,kwa maana ya kuhimiza wananchi kuendelea kusafisha na kutunza maeneo yao ya kazi,na tunaona elimu ambayo wameitoa,imekuwa ikizaa matunda kwani  kuna jitihada ambazo zimeendelea kufanyika hasa za kusafisha maeneo hayo,na kuandaa miundombinu  ya kuhakikisha kwamba maji machafu hayatiririshwi ovyo katika maeneo ya soko,jitihada hizi za usafishaji na utunzaji wa mazingira ziendelezwe.


Vilevile tumeona tayari kuna vyoo vimejengwa pale, kama miundombinu ya soko,na  'tank' kwa ajili ya kumwaga maji machafu ujenzi wake unaendelea, lakini muhimu zaidi ambacho tunasisitiza ni kwamba tunapenda kuona  Wananchi wanaofanya shughuli zao za kila siku katika eneo lile  wanaendelea kuhakikisha kuwa mazingira yao yanakuwa safi muda wote,kwa sababu wanahudumia watu.Afya ya watu ni kipaumbele kwetu sisi,na wananchi wote kwa ujumla."


Wakili huyo amesema kwamba hatua  iliyofikiwa katika usafishaji na utunzaji wa mazingira ya eneo hilo ni nzuri,japo bado haijafikia shabaha  kubwa sana.


Ametoa wito kwa viongozi kuendelea kuwakumbusha Wananchi wajibu wao wa kusafisha na kuhifadhi mazingira, kuendelea kuwaelimisha, kuendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili hali ya usafi katika eneo hilo,pamoja na maeneo mengine, iendelee kuimarika.


Kadhalika ameupongeza uongozi wa serikali ya Mtaa na Kata pamoja na viongozi wote wa wilaya ya Temeke kwa jinsi wanavyoendelea kuwahimiza Wananchi kufanya usafi.


Aidha  ameomba ushirikiano uliopo kati ya sekta Binafsi,Mashirika na Serikali uendelee kuwepo, ili kwa pamoja waendelee kuhimiza suala la usafi na utunzaji wa mazingira.


Katika hatua nyingine mtendaji wa kata ya Mbagala kuu, ndugu  Beatus Kachenje amewashukuru LEAT kwa kuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali za kimazingira,ambapo amesema yeye pamoja na watendaji wote wa Temeke wataendelea kushirikiana nao,na kwamba anaamini kuwa kwa jitihada zinazoendelea kufanyika sasa,kwa siku za usoni Temeke itakuwa katika kiwango kizuri sana cha usafi.


Naye mwenyekiti wa mtaa wa Mbagala Kuu Mashariki,ndugu Fabian  Chilumba  amesema kwamba ziara ya Maafisa hao wa LEAT katika mtaa wake,italeta matokeo makubwa,kwa sababu pamoja na jitihada zote wanazoendelea kuzifanya  ili kuweka mazingira katika hali ya usafi,lakini wakati mwingine wananchi wanahitaji kuona sura tofauti,na kusikia sauti tofauti,ili kuhamasika zaidi kufanya jambo fulani.


LEAT ni shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa rasilimali za Maliasili.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke