• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Kamati ya Mazingira Yafanya Ziara Kata ya Kijichi.

Posted on: April 21st, 2021

Wajumbe wa kamati ya Mazingira ya wilaya ya Temeke  wakiwa katika kikao kifupi kabla ya kuanza ziara ya ukaguzi wa maeneo yenye changamoto za kimazingira katika mitaa ya Misheni na Kijichi.Kikao hicho kimefanyika katika ofisi ya Mtendaji wa kata ya kijich.Ziara  imeandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Lawyer's Environment Action Team(LEAT) .Aliyesimama ni Meneja mradi  Bibi Teresia Fabian  akizungumza na kamati wakati wa kikao hicho.



Kamati ya mazingira wilaya ya Temeke kwa kushirikiana na asasi isiyokuwa ya kiserikali ya lawyer's Environment  Action Team (LEAT) wamefanya ziara katika mitaa miwili ya kata ya Kijichi ambayo ni  Misheni na Kijichi.Ziara hiyo imefanyika leo majira ya saa tano asubuhi.

Ziara hiyo ni maatokeo ya kikao cha kamati za mazingira Mkoa wa Dar es Salaam cha tarehe 15/04/2020 kilichoandaliwa na LEAT ambapo katika kikao hicho  LEAT ilipendekeza kufanyika kwa ziara,katika maeneo mbalimbali ya mkoa  huo kwa lengo la kuendelea kubaini changamoto za kimazingira zilizopo katika maeneo hayo na kuzitafutia ufumbuzi.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo ,Afisa Mazingira wa Manispaa ya Temeke bibi Fina Benard  amesema kwamba  katika ziara hiyo kamati imebaini changamoto ya kuwepo kwa taka ngumu katika maeneo waliyotembelea.

''Changamoto kubwa katika eneo la  Misheni ni taka ambazo zinazalishwa  na wafanyabiashara waliopo katika eneo hilo ,pamoja na baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo,ambao nyakati za usiku hutoa taka majumbani na kuzipeleka katika eneo hilo.Uongozi kwa kushirikiana na wafanyabiashara hao wameshapata ufumbuzi wa changamoto hiyo ,mkandarasi amepatikana,taka hizo zinazolewa kila siku''.Alisema Fina.

Kuhusu mchango wa LEAT  katika utatuzi wa  changamoto za kimazingira wilayani Temeke,Fina  amesema ''LEAT wamefanya kazi kubwa sana,kwanza walianza kutoa elimu kwa watendaji wa kata na mitaa tofauti tofauti,wameshatupa elimu sisi maafisa mazingira,kama mjuavyo elimu haina mwisho,lakini pia baadhi ya wenyeviti wa mitaa,wamachinga,baba lishe na mama lishe wamepewa elimu juu ya utunzaji wa mazingira, na uhifadhi wa taka.Tunaomba  waendelee kutupa elimu, Kwa msaada wao LEAT ,pamoja na juhudi zinazofanywa na Manispaa, tunaamini kwamba ipo siku tutafika sehemu ambayo tunahitaji kufika.

Kwa upande wake  mwenyekiti wa mtaa wa Kijichi ndugu Mohamed Rajabu ameeleza kuhusu changamoto ya daraja la Kijichi ambapo  mvua zinaponyesha mchanga mwingi huletwa na maji katika eneo hilo,mfereji kujaa mchanga hadi kufikia usawa wa daraja,hali ambayo inasababisha usumbufu kwa wananchi.Mohamed Rajabu amesema kwamba serikali imejipanga kutatua kero hiyo  kupitia Mradi wa DMDP ,daraja hilo litajengwa mwakani.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Misheni  ndugu  Bakari Masasi amesema kwamba changamoto ya kimazingira iliyopo katika mtaa wake  ni ukusanyaji wa taka  katika kituo cha daladala cha Misheni.Kuhusu juhudi za serikali katika kutatua changamoto hiyo,Masasi amesema kwamba pamoja na eneo hilo kutokuwa rasmi kwa ukusanyaji wa taka,lakini uongozi wa mtaa pamoja na wafanyabiashara wa eneo hilo wameweka utaratibu kuhakikisha kwamba kila siku gari la taka linafika katika eneo hilo na kuzoa taka zote.

LEAT  imekuwa msaada mkubwa katika kuisaidia serikali kutatua changamoto za kimazingira,ziara hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa  kazi za mradi wa kulinda haki za kimazingira kwa wanawake,vijana, wasichana na jamii kwa ujumla kwa kuiwezesha jamii katika masuala ya kisheria,kutambua haki zao za kimazingira,na kuishi katika mazingira safi na salama,mradi ambao unatekelezwa  na LEAT kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la 'Legal Services Facility'.



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke