• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

KAMATI YA USEMI KUHAKIKISHA BILIONI 20 ZINAREJESHWA HALMASHAURI

Posted on: October 15th, 2022

Leo Oktoba 15,2022 kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) ikiongozwa na mwenyekiti ambaye ni mbunge wa jimbo la Temeke mheshimiwa Abdallah Chaurembo imefanya kikao cha majumuisho ambapo wajumbe wa kamati hiyo kwa pamoja wameazimia kuokoa shilingi Bilioni 20 zilizopotea kutoka kwenye mikopo ya  Wanawake,Vijana na watu wenye Ulemavu maarufu kama "mikopo chechefu" kutokana na wakopaji kutorejesha mikopo yao.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Chaurembo alisema

"Ndani ya mwezi mmoja Ubungo wameweza kurudisha milioni 161, tunaamini asilimia kubwa ya fedha hizi zitarudi, Temeke nao wamefanya namna ya kurudisha vifaa vya kilimo vilivyotolewa kwa kikundi fulani na vinafanyiwa utaratibu mwingine na havitapoteza thamani, ile milioni 175 itarudishwa kwenye mfuko wa maendeleo ya Wanawake,Vijana na na Watu  wenye ulemavu, hivyo hivyo kwa Halmashauri zingine"

Aidha Mhe. Chaurembo alieleza kuwa Halmashauri zimeanzisha utaratibu wa kutuma message za kukumbusha 'Push Button' kila mwezi kwa wadaiwa ambapo itasaidia kuhamasisha wadaiwa kulipa madeni yao, na kusisitiza mikopo kutolewa kwa vikundi vyenye tija.

"Tumekuja na utaratibu wa 'Push button' tunaamini hautatumia gharama kubwa na utasaidia kuwakumbusha wadeni kufanya marejesho yao. Kwa mwaka huu, mikopo ikatolewe kwa vikundi vyenye tija, kwa mfano wenzetu hapa Ilala, wameanzisha kikundi cha lishe chenye tija na kipo 'committed', hii ni fursa kwa Halmashauri kuona na kujifunza lakini pia Wakurugenzi na Maafisa Maendeleo ya Jamii wajifunze hata wao wenyewe kwa wenyewe ili kubadilishana uzoefu, sio lazima tutoke nje ya Nchi, tunaweza kusaidiana wenyewe kwasababu wapo wanaofanya vizuri zaidi"

Aidha Mhe. Chaurembo amesisitiza kuwa fedha zote za Serikali zisimamiwe kwa makini kuhakikisha zinaenda kutimiza lengo lililokusudiwa na kuwasaidia Wananchi wanaostahili.

"Fedha zote za Serikali zilizoletwa zisimamiwe kwa makini kuhakikisha zinaleta tija, kamati yetu imedhamiria kumsaidia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, tumeondoka na majina ya vikundi vyote chechefu tutaendelea kuvifuatilia kuhakikisha Bilioni 20 zinalipwa, niwahakikishie bilioni 68 zinazokwenda kutolewa mwaka huu zitakopeshwa kwa weledi na Watanzania watafaidika" alisisitiza Mhe. Chaurembo.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi Idara ya Serikali za Mitaa TAMISEMI Angelista Kihaga, ameishukuru kamati hiyo kwa kuwa na manufaa kwa jiji la Dar es Salaam.

Kamati ya USEMI ni kamati ya kudumu ya Bunge inayosimamia masuala mbalimbali ya Serikali za Mitaa, na inalenga kuhakikisha maendeleo yanapatikana na yanasimamiwa ili kuwa Endelevu kwa faida ya Taifa ambapo kwa sasa inasimamia mchakato wa kurejesha fedha za mikopo ya 10% ambazo hazijarejeshwa kwa mkoa wa  Dar es Salaam

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke