• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

'Lawyers Environment Action Team' (LEAT) Wadau Muhimu Katika Utatuzi wa Changamoto za Kimazingira Temeke.

Posted on: January 19th, 2021

Wahe. Madiwani  na Wataalam mbalimbali wa halmashauri  za Mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini kikao maalum cha kuunda kamati za Mazingira za Wilaya kilichoandaliwa na asasi isiyokuwa ya Kiserikali  ya 'Lawyers Environment Action  Team '( LEAT)

Asasi ya 'Lawyers Enivironment Action Team'(LEAT) kupitia mradi wake wa kulinda haki za kimazingira kwa wanawake ,vijana ,wasichana na jamii kwa ujumla  kwa kuwezesha jamii katika  masuala ya kisheria,mradi ambao unatekelezwa kwa ufadhili wa shilika lisilo la kiserikali la 'Legal Services Facility', imedhamiria kushirikiana na jamii kutatua changamoto za Kimazingira.

Lengo likiwa ni  kuwajengea uwezo wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam  kuelewa na kutimiza wajibu wao ili kuishi katika mazingira safi na salama.

Katika kuhakikisha kuwa inafanikiwa kufikia lengo, LEAT imeweka mikakati mbalimbali ,moja  ya mikakati hiyo ni uanzishaji wa kamati za Mazingira za Wilaya,ambapo kamati hizo zinaundwa na watu 7 ambao ni  Madiwani 2,Maafisa Mazingira 2,Afisa mtendaji wa Kata 1,Afisa Maendeleo ya Jamii 1 na Afisa Habari 1 .

Baada ya kuundwa kwa kamati hizo,jukumu la kwanza la kamati kwa kushirikiana na wataalamu  wa LEAT,lilikuwa ni kuainisha maeneo yenye changamoto kubwa za kimazingira kwa wilaya zote,na baada ya kuainisha,waliweka azimio la pamoja,ambalo ni maafisa wa LEAT,Kamati na Wenyeviti wa Mitaa kutembelea maeneo hayo.

Wilaya ya Temeke  kama ilivyokuwa kwa wilaya nyingine za mkoa wa Dar es Salaam, Januari 18 ,2021, majira ya saa tano asubuhi, ilifikiwa na ugeni huo wa LEAT ,huku eneo lengwa likiwa ni kata ya Charambe,iliyopo katika tarafa ya Mbagala.Na kama ilivyo ada  Maafisa hao waliungana na kamati ya mazingira ya Wilaya,Wenyeviti wa Mitaa na Afisa Afya wa Kata , wote kwa pamoja walitembelea mitaa ya Kurasini mji mpya na Rangi Tatu.

Baada ya kujionea hali ya mazingira ilivyo katika mitaa hiyo,  mratibu wa mradi bibi Teresia Fabian alikuwa na haya ya kusema''Leo tumefika katika kata ya Charambe,tumetembea mitaani, tumejionea hali halisi,mara baada ya kukamilisha ziara katika wilaya zote ,tutakaa pamoja, tujadiliane namna tutakavyoweza kutatua changamoto ambazo wote hapa tumezishuhudia''.

Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Rangi Tatu ndugu Hafidhi Chaukulu  alisema kwamba changamoto za Kimazingira katika mtaa wa Rangi tatu ni kubwa,jitihada nyingi zimefanyika kuhakikisha kwamba hali ya usafi wa mazingira inakuwa bora.

Akizungumza kuhusu juhudi zilizokwisha kufanyika na muitikio wa wananchi Chaukulu alisema''mkuu wa wilaya ya Temeke mheshimiwa Godwin Gondwe  alizindua kampeni ya usafi ya Wilaya,na baada ya uzinduzi huo alitoa maelekezo kwamba kila Jumamosi iwe ni siku ya usafi.Sisi kama serikali ya mtaa  tunasimamia maelekezo hayo,na tangu agizo hilo lilipotolewa, wananchi wamepata mwamko ,wanafanya usafi, japokuwa  bado hatujafikia kiwango kinachotakiwa,lakini kuna mabadiliko makubwa. Tunaendelea kutoa elimu pamoja na kuwahimiza wananchi kufanya usafi.Ujio wa LEAT leo umetupa hamasa zaidi.Naamini kwamba kwa kushirikiana nao, tutafika pazuri.

Suala la usafi wa mazingira linahitaji nguvu ya pamoja,serikali peke yake haiwezi, kwa sababu ina majukumu mengi.Lakini wanapotokea wadau kama hawa ,na jamii ikashirikishwa kwa karibu,mazingira yetu yatakuwa safi.LEAT ni wadau muhimu sana ,ni matumaini yangu kwamba watatusaidia kutatua changamoto za kimazingira zinazotukabili ndani ya wilaya Yetu''.

Katika hatua nyingine Afisa Afya wa kata ya Charambe bibi Shufaa Msangi alibainisha sababu za uchafuzi wa mazingira katika kata hiyo ,sababu hizo ni ;Idadi kubwa ya wafanyabiashara ndogondogo(Wamachinga) wanaofanya biashara zao pembeni mwa barabara,mama lishe ambao hufanya biashara zao nyakati za usiku ,ambapo  baada ya kumaliza shughuli zao  humwaga maji machafu na mabaki ya vyakula katika mifereji ,Baadhi ya mifereji kutokuwa na muunganiko, hali ambayo inasababisha maji kukosa uelekeo na kuishia kwenye barabara za mitaani, pamoja na mifereji  kutokuwa na mteremko , hali ambayo  inasababisha maji kutuwama wakati wote.

'Lawyers Environment Action Team'(LEAT) ni asasi isiyokuwa ya kiserikali.inayojihusisha na ulinzi na utunzaji wa mazingira.ilianzishwa mwaka 1994.Makao makuu ya asasi hii yapo Mikocheni jijini Dares salaam.LEAT  ina matawi  katika mikoa miwili ambayo ni Iringa na Rukwa.lakini,inafanya kazi katika mikoa yote ya Tanzania.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke