• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

LEAT YATUA KILUNGULE

Posted on: August 24th, 2021


Maafisa kutoka katika asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Wanasheri Watetezi wa Mazingira (LEAT) kwa kushirikiana na kamati ya mazingira wilaya ya Temeke imefanya ziara ya ukaguzi wa Mazingira katika kata ya Kilungule.Ziara hiyo imefanyika leo Agost 24,2021 majira ya saa tano asubuhi.

Katika ziara hiyo kamati pamoja na maafisa hao walitembelea maeneo mbalimbali yenye changamoto za kimazingira likiwemo eneo la makaburi lililopo katika mtaa wa Kilungule ambapo changamoto inayolikabili eneo hilo ni mmomonyoko wa udongo ambao umesababisha sehemu  ya makaburi hayo kumegeka, hivyo  baadhi ya makaburi kupotea.

Akizungumza mara baada ya kuupokea Ugeni huo diwani wa kata hiyo Mheshimiwa Said Fella amesema kwamba kata ya Kilungule ina changamoto kubwa za kimazingira ,na moja ya sababu kubwa ya uwepo wa  changamoto hizo ni jiografia ya kata hiyo,ambapo imezungukwa na mabonde.Amesema  anatamani kuona matokeo ya ziara hiyo,kwamba yatapunguza changamoto zilizopo,ambazo kutokana na asili yake,utatuzi wake unahitaji fedha nyingi.

Aidha mtendaji wa kata hiyo bibi Edith Kwai amesema kwamba msimu wa mvua nyingi maji kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Temeke hupita katika eneo hilo,na kwa sababu  sehemu kubwa imezungukwa na mabonde,sehemu kubwa ya eneo hilo imekuwa ikikumbwa na tatizo la mmomonyoko wa ardhi ,ambapo uongozi wa kata umefanya jitihada mbalimbali kupunguza athari zinazotokana na  hali hiyo,lakini kwa kiasi kikubwa bado ni   changamoto.


 LEAT kupitia mradi wake unaolenga kuwawezesha wakazi wa jiji la Dar es Salaam kutambua haki yao ya kuishi katika mazingira safi na salama, iliunda kamati za watu 7 kwa kila wilaya , maafisa  wa LEAT kwa kushirikiana na kamati hizo wamekuwa wakifanya ziara kutembelea maeneo mbalimbali yenye changamoto za kimazingira, kuangalia changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi , ziara ya leo ni muendelezo wa ziara hizo,ambapo baada ya kuhitimisha kamati zote zitakutana  kujadili kwa pamoja na kutafuta masuluhisho.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke