• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

MKURUGENZI TEMEKE AUNGANA NA JESHI LA POLISI KUMWAGA ZEGE LUMO SEKONDARI

Posted on: January 23rd, 2023

Na: Sweetbetter Njige

TMC Habari


Januari 23,2023 mkurugenzi wa manispaa ya Temeke ndugu Elihuruma Mabelya ameungana na jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Temeke  kumwaga zege ikiwa ni hatua za awali za ujenzi wa madarasa ya ghorofa yanayojengwa katika shule ya sekondari Lumo iliyopo katika kata ya Yombo Vituka.

Akizungumza katika zoezi hilo mkurugenzi Mabelya amelishukuru Jeshi hilo kwa kufanya maamuzi ya kushirikiana na jamii katika ujenzi wa madarasa hayo,alisema.

"Jeshi la polisi limetoa mchango wa nguvu kazi katika ujenzi wa madarasa haya.Tukio hili ni la kuigwa, sisi kama Halmashauri tumelipokea kwa mikono miwili, hii ni dhana ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa vitendo,hii ndio maana ya 'Kazi Iendelee'

Aidha mkurugenzi Mabelya ametoa wito kwa taasisi na mashirika mbalimbali kuunga mkono jitihada za Serikali kushiriki katika shughuli za kijamii hususani katika shughuli za kuboresha sekta ya elimu.

"Niombe mashirika na taasisi mbalimbali katika halmashauri yetu, kujitokeza kwa wingi kushiriki na kurudisha kwa jamii kwa kutoa sehemu ya faida yao au nguvu kazi ili kumuunga mkono mheshimiwa Rais hasa katika kipindi hiki anachojitoa kuwekeza katika sekta ya elimu, niwaombe tuige mfano huu uliooneshwa na Jeshi la polisi"

Kwa upande wake ACP John Malulu ameeleza furaha yake katika kushiriki zoezi hilo kama Maaskari na Wazazi.

"Tumekuja hapa kuunga mkono kazi nzuri ya Serikali yetu katika kuhakikisha watoto wa Temeke wanapata mahali pa kusoma, tutambue askari wa Temeke ni sehemu ya wana Temeke, tumeona ni muhimu kuja kuchangia nguvu kazi  za mikono hapa kwakua watoto wakielimika watapata maarifa ya kufanya shughuli zao maalumu za kujitegemea na tutaondoa uhalifu"

Manispaa ya Temeke inatekeleza mradi wa vyumba 32 vya madarasa vinavyojengwa kwa mtindo wa ghorofa katika Shule ya Sekondari Lumo ambapo kwa sasa ujenzi upo katika hatua za mwanzo na unatarajiwa kukamilika mapema mwezi Machi,2023.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke