• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

MAADHIMISHO YA MIAKA 45 YA CCM WILAYA YA TEMEKE YAFANYIKA KIBURUGWA

Posted on: February 3rd, 2022


MAADHIMISHO YA MIAKA 45 YA CCM WILAYA YA TEMEKE, YALIYO FANYIKA KATA YA KIBURUGWA .

Maadhimisho hayo yalianza saa mbili kamili kwa matembezi ya mshikamano,kutoka barabara kuu ya Mbagala hadi ofisi za Kata ya Kiburugwa zilipo zilipofanyika shamra shamra za maadhimisho hayo.

Matembezi hayo yaliongozwa na  Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,  Adamu Ngarawa akimwakilisha mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mama Kate Kamba, Mwenyekiti wa CCM, Temeke Almishi Hazal, Katibu Kitte Adamu Mfilinge.

Pia Mkuu wa Wilaya Jokate Mwegelo ni moja ya viongozi walio shiriki katika maadhimisho hayo.

 Maadhimisho hayo yalipambwa kwa burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na Msagasumu, vikundi vya taarabu na ngoma za asili.

Awali vijana wa chipukizi walimkabdhi Katibu  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Adamu Ngarawa Picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, Hayati Mwalimu Julias Nyerere, na bendera ya CCM naya Tanzania.

Katika hotuba yake Katibu Adamu Ngarawa  aliipongeza Wilaya ya  Temeke kwa maadhimisho hayo mazuri ya miaka 45 ya kuzaliwa CCM.

Pia aliwapongeza viongozi wa Temeke kwa kusimamia vyema maendeleo makubwa katika Wilaya  hiyo, ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali ya elimu, afya na barabara akitolea mfano kituo cha afya cha Buza.

Katibu Adamu Ngarawa alisema katika kuadhimisha  miaka 45 ya  CCM, Tanzania inajivunia mafanikio makubwa ya miundombinu bora ya elimu, iliyojengwa na  Rais Samia Suluhu Hassan kwa muda mfupi alioingia madarakani.

Alisema kwa kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia ya kujenga miundo mbinu, watahakikisha wanasimamia vyema maendeleo ya elimu ilikuongeza ufaulu kwa shule za Serikali na kufuta zero.

Alisema vyumba vya madarasa vilivyojengwa na Rais Samia vimeweke rekodi kwa ubora, hivyo hawatavumilia mzazi asiyepeleka mtoto wake shule kwa kuwa madarasa yapo yakutosha.

" Niwatake mabalozi wa nyumba kumi kuhakikisha wanakagua kila nyumba, kuona kama kuna mzazi yeyote ambaye hakumpeleka mtoto wake shule aliyefaulu ili achukuliwe hatua," alisisitiza.

Katibu Adamu Ngarawa alisema watoto kutopelekwa  shule ni chanzo cha kujiingiza katika vitendo vya uharifu ikiwemo ukabaji, hivyo wazazi lazima wahakikishe watoto wao wote wanapata haki yao ya kieleimu.

Alisema watoto hao wakipata elimu watakuwa msaada mkubwa kwa jamii katika taaluma mbalimbali,ikiwemo uwalimu, utabibu na viongozi katika nyadhifa mbalimbali.

Akizungumzia uchaguzi wa Chama, aliwataka wanachama kuendelea na zoezi la kujisajiri kwa njia ya kielektroniki matawini.

Pia aliwaagiza viongozi wa Temeke kushirikiana ilikuongeza vitendea kazi simu janja kwaajili ya kurahisisha zoezi la kusajiri wanachama.

Alisema wao kama viongozi wamejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa wa haki kwa kila mmoja, wanapinga rushwa na upendeleo, bali kila mmoja atachaguliwa kwa sita zake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Temeke, Almishi Hazali alisema alimpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi za maendeleo katika Wilaya hiyo, ambazo zimejenga miundo mbinu mingi ya elimu na afya.

" Tunazidi kufanya kazi kwa juhudi ikiwa nisehemu ya kumuunga Rais Samia mkono katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoinua uchumi wa kila mtanzania," alisema.

Naye Mkuu wa Wilaya Jokate Mwegelo alisema wataendelea kudumisha ushirikiano ili kuijenga Temeke mpya ya mfano katika Wilaya zote za Dar es Salamaam.

" Tunatambua pamoja na mambo makubwa yanayofanywa na Rais Samia katika Wilaya yetu, bado zipo changamoto ndogondogo hivyo tutaendelea kushirikiana na viongozi wenzangu ilikuzitatua kwa wakati," alisema.

Pia Jokate alisema wataendelea kujenga na mpango wa kujenga shule za Sekondari katika kata sita ambazo hazijajengewa shule hizo.

Naye Katibu wa CCM, Wilaya hiyo Kitte Mfilinge aliwapongeza viongozi na wanachama kwa kujitokeza katika maadhimisho hayo ya wilaya, nakuwaahidi utekelezaji mzuri wa ilani ya Chama.

Katibu Kite alisema Mambo mengi yanazidi kufanyika katika Wilaya hiyo ikiwemo vijana kupewa mikopo ya asilimia kumi isiyo na riba na kuboresha mifumo ya elimu na miundo mbinu.

" Sisi viongozi wa chama tuko imara kuendeleza jitihada na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia watanzania wote hasa wanatemeke," alisema Kite.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke