• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Madiwani Temeke Waitaka Serikali Kuweka Mkazo kwenye viwanda vya Zamani

Posted on: May 31st, 2019

Naibu Mstahiki Meya wa halmashauri ya manispaa ya Temeke  Mhe. Juma Rajab Mkenga akizungumza wakati wa ziara ya madiwani  kutembelea viwanda.

Wahe. madiwani pamoja na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali vya halmashauri ya manispaa ya Temeke  wakiwa katika ziara ya kutembelea viwanda .

Wahe. madiwani wa manispaa ya Temeke wakisikiliza maelezo  kuhusu namna uzalishaji  vilainishi unavyofanyika katika kiwanda  cha General Petroleum Ltd (GP).

Wafanyakazi wa kiwanda cha General petroleum (GP) wakiwa katika hatua ya kuweka vilainishi katika vifungashio.



..................HABARI KAMILI...................




Naibu Mstahiki Meya wa halmashauri ya manispaa ya Temeke Mhe. Juma Rajab Mkenga  ameitaka serikari  kuweka mkazo mkubwa kwenye viwanda vya zamani ambavyo vinaendelea kufanya uzalishaji  ili ajira zinazotolewa na viwanda hivyo ziendelee kulindwa.Mh. Mkenga ameyasema hayo mapema leo Ijumaa  wakati wa ziara ya Waheshimiwa madiwani kutembelea viwanda.

Akizungumza katika mahojiano mafupi   Mhe Mkenga anasema''Sisi tunafanya ziara kutembelea viwanda, lakini hatutembelei  kama watendaji wa serikali,  tunaangalia jinsi viwanda vinavyofanya kazi,tuone je uwepo wa viwanda hivi unatimiza malengo yaliyokusudiwa ya kutupeleka kwenye uchumi wa kati?Je viwanda hivi vinatoa ajira kiasi gani kwa wananchi wetu?Kwa sababu sera ya Mhe. Rais ni ujenzi  wa viwanda,kukuza uchumi wa nchi kupitia viwanda.Sasa tunaanzisha viwanda vipya,je viwanda vya zamani hali yake ikoje?Je vinafanya kazi? Je bado vinauwezo wa kujiendesha kwa faida.Je upo uhakika wa ajira endelevu  katika viwanda hivyo?''.

Mhe. Mkenga amesema  nia hasa ya ziara hiyo ni kutaka kujua  matatizo yanayowakabili  wamiliki wa viwanda vya zamani , waishauri serikali iyashughulikie,ili  matatizo hayo yasiendelee kujitokeza kwenye viwanda vipya vinavyoendelea kuanzishwa.Amesema wao kama madiwani wanawajibika kuiambia serikali  kuhusu  matatizo  yanayowakabili wawekezaji katika sekta ya viwanda.

Naye diwani wa kata ya Kilungule Mhe. Said Hassan Fella amesema kwamba katika ziara hiyo  wanakutana na wamiliki wa viwanda kuzungumza nao ili kubaini changamoto zao,kadhalika wafanyakazi wa viwanda hivyo .Na katika kuhakikisha kwamba changamoto zitakazobainika zitafanyiwa kazi, wameambatana na watendaji ambao ni wakuu wa idara mbalimbali za manispaa ili watakapokuwa wanakaa  katika kamati zao,  na katika baraza, wakizungumza kuhusu changamoto za viwanda wawe wanazungumza lugha moja. Mhe. Fella pia amesema kwamba lengo la ziara hiyo ni kuangalia kuhusu ushirikiano baina ya viwanda hivyo na manispaa hususani kwenye kulipa tozo za manispaa, kama zinalipwa kwa wakati, na kama kuna changamoto zozote zinazotokana na tozo hizo.

Aidha diwani wa kata ya Mbagala kuu Mhe. Shabani Othman Abubakari amesema kwamba wao kama madiwani wameamua kutembelea viwanda kwa sababu viwanda ndio sera inayotekelezwa sasa na serikali ya awamu ya tano.Vile vile kwa kutembelea viwanda wameona jinsi viwanda vinavyofanya kazi,Wamefahamu changamoto zilizopo viwandani,hivyo baada ya ziara hiyo watakaa wajadili ni namna gani ya kuwasaidia wamiliki wa viwanda hivyo kutatua changamoto  kwa sababu  wamiliki hao wanalipa kodi,wakipata hasara hawataweza kujiendesha,hawatalipa kodi, manispaa itakosa gawilo lake linalotokana na tozo.Si hayo tu ,lakini pia kuangalia ni kwa namna gani manispaa inaweza kuingia ubia katika baadhi ya viwanda,ili iweze kupata mapato makubwa zaidi ,kuliko inavyopata sasa .

Katika hatua nyingine wamiliki wa viwanda vilivyotembelewa wameeleza changamoto wanazokabiliana nazo katika uendeshaji wa viwanda vyao,lakini pia hawakusita kueleza kuhusu ushirikiano wanaoupata kwa mkurugenzi pamoja na Mhe. Mstahiki Meya pale wanapowaeleza  kuhusu changamoto hizo.

Katika ziara hiyo ya siku tatu ambayo imehitimishwa leo,Waheshimiwa madiwani wametembelea viwanda mbalimbali vilivyopo ndani ya manispaa ya Temeke vikiwemo kiwanda cha Berger Tanzania Limited ambao ni wazalishaji wa rangi na kiwanda cha  kutengeneza vilainishi  cha General Petroliam Limited(GP).




.............MWISHO...................


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke