• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia aleta neema TASAF.

Posted on: November 16th, 2018

Mpango wa kunusuru kaya masikini katika mtaa wa Mamboleo B kata ya Sandali, ni moja ya mpango wa kuziwezesha kaya masikini sana kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji ya msingi, pia kuwekeza kwenye rasilimali watu  kwa kuwapa ruzuku ya masharti kwa Wananchi hususan kwa watoto wanaotakiwa kwenda shule na wanaotakiwa kuhudhuria kliniki.

Halmashauri ya Temeke kupitia mratibu wa TASAF Bibi Tatu, alisema wamewezesha na kuwasaidia walengwa kupitia pesa wanazolipwa kuweka akiba,kukopeshana na kuanzisha biashara mbalimbali ambazo zitawasaidia kujikwamua kimaisha na kuelezea mpango huu ulioanzishwa rasmi mwaka 2015.

Nae mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ndg,Joel  Mwakabibi aliwaelezea wageni kwamba serikali ya awamu ya tano ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imejikita na kujizatiti kupunguza/kuondoa umasikini kwa watu wake kwa kujenga nchi ya viwanda.

“Nimefurahishwa na walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini,wameanza kwa nguvu na staili ya aina yake  ya kuanzisha viwanda vidogovidogo ambavyo vinaongeza kipato cha kaya zilizo kwenye mpango na hata ambazo hazipo kwenye mpango”alisema

Sambamba na hilo amezisifu kaya ambazo hazipo kwenye mpango kwakuwa zimepata ajira na huduma toka kwa kaya hizi ambazo ziliitwa kaya masikini kabla ya kuanza kwa mpango huu.

Akimkaribisha Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia , kwa Kanda ya Afrika alisema kwa sasa TASAF imepanua wigo na kwa awamu ya tatu kila kijiji kitapewa ruzuku kama motisha ili kuhakikisha tunapunguza umasikini.

“Huwezi kutokomeza umasikini  kwa kutoa ama kugawa fedha bali kwa kujishughulisha ili kujikwamua na umasikini”alisema

Mratibu wa TASAF wa Manispaa ya Temeke Bibi Tatu alisema pamoja Na kuwepo kwa mafanikio katika kaya masikini sana,bado kumekuwepo  na kaya masikini ambazo hazikuandikishwa kwenye mpango kwasababu mbalimbali,pia kuna ushindani mkubwa wa masoko pamoja na kutokujua  kusoma na kuandika kwa baadhi ya walengwa.

Akihitimisha alisema”TASAF awamu ya tatu imeendelea kufanikiwa kutokana na ushirikiano wa kiutendaji katika ngazi mbalimbali za utekelezaji kuanzia Taifa hadi ngazi ya Jamii,na kuwashukuru TASAF makao makuu,ofisi ya  Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke,viongozi wa kata,viongozi wa dini na vyama mbalimbali na wananchi kwa ujumla.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke