• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

MANISPAA YA TEMEKE YAPOKEA KIANZIO CHA UJENZI WA HOSTELI ZA WANAFUNZI WA KIKE MKOA WA DSM

Posted on: January 19th, 2024

Na: Joanita Joseph -TMC Habari


Katika kuunga mkono juhudi za serikali hususani kwenye uboreshaji wa miundombinu ya elimu hapa Nchini, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila januari 19, 2023 katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa ujenzi wa hostel mkoa wa DSM ameikabidhi halmashauri ya manispaa ya Temeke mabati na fedha kiasi cha shilingi Milioni 20 zitakazotumika kama kianzio cha ujenzi wa hostel (daharia) kwa wanafunzi mkoa wa Dar es salaam.


Akizungumza wakati wa hotuba yake Mhe. Chalamila amesema kuwa mpango huo utaanza na ujenzi wa hostel za kike ili kuwaondolea mazingira hatarishi na changamoto hasa wanapotoka mbali kuja kufata elimu.


"Mtoto wa kike lazima awe katika mazingira mazuri sana ya kumlinda kwakuwa ndiye aliyebeba kizazi cha kesho, tukiwekeza kwa msichana kuanzia sasa maana ake tutapata kizazi kilicho bora kwasababu watu wote watakuwa wamekaa kwenye tumbo lililo salama" alisema Mhe. Chalamila.


Mhe. Chalamila ameitaka kila halmashauri kuandaa harambee (fundraising) kwa ajili ya kupata vifaa vya kuendeleza ujenzi, kuja na mpango kazi maalum na kutoa fedha pamoja na kuchora ramani ya jengo la hostel itakayowezesha kubeba wanafunzi wasiopungua 80 mpaka 120 kulingana na taratibu za TAMISEMI ambapo atakuja kuichagua ramani ya mfano pindi atakapokuja kugawa fedha kwa awamu ya pili.


Halkadhalika, amemtaka kila Mkuu wa wilaya kuunda timu ndogo ya kufatilia wajibu wa kurudisha kwa jamii (Corporate Social Responsibility) kwenye eneo lake ambayo kipaumbele chake kitakuwa ujenzi wa hostel hiyo.


Aidha Mhe. Chalamila amesema kuwa mkoa wa DSM unaandaa utaratibu wa harambee ambapo watapata changizo kubwa kutoka kwa wadau na fedha hizo zitaelekezwa kwenye halmashauri zote.


Nae Ndg.Elihuruma Mabelya, mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi amehaidi kutekeleza kwa vitendo maagizo hayo ikiwemo kutafuta wadau wa kuwaunga mkono katika kufanikisha jambo hilo muhimu.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke