• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Mhe Kandege Naibu waziri OR-TAMISEMI aipongeza Manispaa ya Temeke kwa kuchapa kazi.

Posted on: June 24th, 2020

NAIBU WAZIRI OR-TAMISEMI MHE JOSEPHAT KANDEGE AFANYA ZIARA MANISPAA YA TEMEKE

Naibu waziri OR-TAMISEMI Mhe Josephat Kandege leo amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

Na kupokelewa na Mkurugenzi wa Manispaa Ndg Lusubilo Mwakabibi pamoja na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri hiyo.

Lengo la ziara yake ni kufuatilia namna manispaa ya Temeke inavyokusanya mapato na matumizi ya fedha hizo zinazotokana na makusanyo hayo katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Naibu waziri OR-TAMISEMI Mhe Josephat Kandege katika picha akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa Ndg Lusubilo Mwakabibi mwenye kofia akimpa maelezo mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha kisasa Yombo vituka Temeke. 

Akiwa katika ziara hiyo Mhe Naibu Waziri ametembelea miradi miwili ambayo ni mradi wa ujenzi wa Kituo cha afya Yombo vituka na Kiwanda cha ushonaji nguo Kibonde maji Temeke.

Mhe Kandege amepongeza namna Manispaa ya Temeke inavyotekeleza miradi ya maendeleo kwa kiwango cha juu kwa kutumia fedha za mapato ya ndani akitolea mfano ujenzi wa kisasa wa  gorofa mbili kituo cha afya Yombo vituka pamoja na utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu ambapo manispaa ya Temeke imekua ikitoa vifaa badala ya fedha.

‘Utaratibu wa utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa kuwapa vifaa ni mzuri kwa kuwa unatengeneza ajira lakini pia urejeshaji wake sio wa mashaka na hata ikitokea wameshindwa kurejesha Manispaa inauwezo wa kuchukua vifaa vyake,” alisema Mhe Kandege.

Aidha akiwa katika kituo cha afya Yombo vituka ameshauri menejimenti ya Manispaa chini ya Mkurugenzi Ndg Lusubilo Mwakabibi kuona namna ya kujenga nyumba za watumishi kwa kuwa eneo lipo, pia kwa upande wa Jukwaa la wanawake JUWATE ambao wanakiwanda cha ushonaji wanufaika wa asilimia 10 ameshauri Manispaa kuwasaidia kupanua soko hususani sare za wanafunzi kwa kuhakikisha sare za wanafunzi wote wa Temeke zinatoka katika kiwanda hicho.

Naibu Waziri TAMISEMI Mhe Kandege akiongea na mmoja kati ya mafundi wa kushona alipozuru Jukwaa la wanawake Temeke (JUWATE) ambao ni wanufaika wa mikopo ya 10% inayotolewa na Manispaa ya Temeke.


Kwa ujumla ameipongeza Manispaa ya Temeke kwa ubunifu, ukusanyaji na usimamizi mzuri wa mapato ya ndani pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa lengo la kuleta ustawi wa wananchi na kuzitaka Halmashauri zingine nchini kuja kujifunza Temeke.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke