• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh.Felix Lyaniva afungua mafunzo ya awali ya usimamizi na ufuatilia wa mikopo bila riba kwa Madiwani

Posted on: March 13th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh.Felix Lyaniva leo amefungua mafunzo ya awali ya usimamizi na ufuatiliaji wa mikopo bila riba kwa waheshimiwa  Madiwani  wa Manispaa ya Temeke.

Alitoa salamu za shukrani kwa ndugu wajumbe wa mafunzo hayo Mh. Lyaniva aliwataka kuzingatia mafunzo hayo kwani ndio chachu ya ukombozi kwa wananchi watakaopelekewa habari hizo za namna ya kujikomboa kiuchumi.

Lyaniva aliwasisitiza waheshimiwa kuhakikisha wananchi katika maeneo yao wananufaika na mikopo hii hususani Wanawake,Vijana na walemavu  kwani hawa ndio walengwa halisi wa mikopo hii.

Nae Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Mh. Abdallah Chaurembo aliwataka wajumbe kuhakikisha vikundi vya ujasiriliamali vinaundwa ili kupata umoja ambao utakuwa ni rahisi kukopesheka.

“Ili kupata mikopo hii kwa urahisi ni vema kuwasisitiza wahitaji kujiunda katika vikundi ili waweze kukopesheka kwa urahisi na iwe rahisi kufanya ufuatiliaji wa ukuaji wa shughuli zao za kujikwamua kiuchumi”alisema

Sambamba na hilo aliwasihi kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa wa biashara wanayotaka kufanya na kuitafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi ya kuchukua mkopo.

Nae mwezeshaji wa mafunzo hayo toka Shule ya biashara Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dr.A.I .Shimba alitoa somo juu ya uendeshaji wa shughuli za ujasiriamali, Umuhimu wa Halmashauri kusaidia wajasiriamali pamoja na faida za ujasiriamali kwa Halmashauri husika.

“Ni vema wajasiriamali wakafanya uchunguzi kuhusu biashara mbalimbali kabla ya kujitosa kuanza kuifanya,hii itasaidia kujua biashara gani  mlengwa ataimudu pindi akipata mkopo wake lakini sambamba na hilo Halmashauri husika ni vema kujiridhisha na wanufaika wa mikopo hiyo ili iwe chachu ya maendeleo katika maeneo yao”

Akihitimisha mafunzo hayo mtaalamu wa ushauri kuhusu masuala ya Mikopo na Ujasiriamali Ndugu J.S.Bwana , alitoa somo juu ya mikopo ya vifaa kwa Wanawake,Vijana na Walemavu katika hatua za kuleta maendeleo endelevu.

‘Ni vema wananchi waelimishwe kuhusu mikopo na aina ya mikopo sambamba na vyanzo mbalimbali  vya upatikanaji wa mikopo ili kuhakikisha mkopo unaelekezwa sehemu sahihi na kuondoa dhana ya majuto pindi mambo yanapoharibika’.Alisisitiza J.Bwana

Naimani muda si mrefu watajitokeza wananchi wakiomba mikopo hii,chamsingi ni vigezo na masharti yazingatiwe ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi wahitaji, na ni vema wawe wahusika halisi wa mkopo huo

“Hakuna kitu kibaya kama kuchukua mkopo bila malengo,ni wazi kuwa baada ya muda majuto yatakukumba tu kwakuwa huna dira katika fedha hiyo,hivyo ni vema kujitathmini unapochukua mkopo unaufanyia nini na wananchi wenu katika maeneo mtokapo muwape elimu hii kabla ya kuamua kuchukua mkopo mahali popote”.

Ndugu J. Bwana alibainisha vifaa vya mkopo vinavyotolewa ni mitambo ya kufyatulia matofali,vyerehani,mashine ya kutengenezea viatu,ununuzi wa bajaji pamoja na Ufugaji  wa  samaki.

Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imejiridhisha na utaratibu  wa mikopo kwa  njia ya vifaa, Hivyo timu ya wataalamu wa Halmashauri itakuwa karibu na waliokopeshwa ili kuhakikisha fedha zinarejeshwa kwa wakati na wakopaji kunufaika na kuhakikisha  miradi inakuwa endelevu kwa kuwezesha ufanisi huo ambao  utaiwezesha Manispaa kutekeleza kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya “ Hapa kazi tu” ikiwa na dhana nzima ya kuwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke