• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Msimamizi wa Uchaguzi Temeke Atoa Maelekezo ya Uchaguzi

Posted on: September 23rd, 2019

Msimamizi wa uchaguzi,ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha sheria,wakili Salum Ally Papen, ametoa maelekezo ya uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa na wajumbe wa kamati za mitaa katika halmashauri ya manispaa ya Temeke.Wakili Papen ametoa maelekezo hayo leo mchana, kwenye ukumbi wa manispaa,mbele ya watendaji wa kata na mitaa.

Katika maelekezo hayo wakili Papen ametaja tarehe ya uchaguzi,mahali uchaguzi utakapofanyika na muda wa uandikishaji ,amesema kwamba uandikishaji wa wapiga kura utafanyika kwa siku 7,ambazo ni kuanzia tarehe 8- 14/10/2019 saa 2:00 asubuhi hadi saa 12 jioni.Uchaguzi utafanyika katika vituo vilevile  vilivyotumika katika uandilishaji wa wapiga kura.

Wakili Papeni amewataka wananchi wote wa manispaa ya Temeke  wenye umri wa miaka 18 na zaidi kushiriki katika uchaguzi.

Kadhalika amewataka wakazi wa Temeke wenye umri wa miaka 21 na zaidi wanaotaka kugombea nafasi ya uenyekiti wa mtaa au ujumbe wa kamati za mtaa kuchukua fomu za kugombea zinazopatikana kwenye ofisi za wasimamizi wasaidizi wa  uchaguzi katika mitaa.

Wakili Papen pia ameelekeza zinapopatikana fomu za kugombea nafasi,ambapo amesema kwamba fomu hizo zitatolewa katika ofisi za wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi katika mitaa kuanzia tarehe 29/10/2019 hadi tarehe 4/11/2019 kuanzia saa 1:30asubuhi ,hadi saa 10:00 jioni.

Aidha wakili Papen ameelekeza kuhusu tarehe za uteuzi,pingamizi,usikilizaji wa rufaa na muda wa kampeni,amesema kwamba uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 05/11/2019 saa 10:00 jioni.Pingamizi dhidi ya uteuzi zitawekwa tarehe 05/11/2019 hadi tarehe 06/11/2019, uwekaji wa pingamizi utakwenda sambamba na usikilizaji wa pingamizi na utoaji maamuzi.Usikilizaji wa rufaa dhidi ya uteuzi utafanyika tarehe 5/11/2019 hadi tarehe 8/11/2019.Mikutano ya kampeni itafanyika kwa siku 7,  tarehe 17/11/2019 hadi tarehe 23/11/2019 ,muda wa kampeni ni saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

Katika hatua nyingine wakili Papen amewataka wananchi wote wa manispaa ya Temeke ambao wana vitambulisho vya kupiga kura,na ambao hawana vitambulisho hivyo  kujitokeza kujiandikisha  katika vituo katika mitaa yao wanayoishi,kwani bila kujiandikisha hawataweza kupiga kura kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa.

Uchaguzi wa serikali za mitaa hapa Tanzania bara utafanyika tarehe 24/11/2019.Kwa halmashauri ya manispaa ya Temeke,uchaguzi huo utafanyika katika mitaa 142.



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke