• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

MSTAHIKI MEYA AHIMIZA ULIPAJI NA UKUSANYI WA MAPATO KWA MAENDELEO YA TEMEKE

Posted on: September 30th, 2023

Na: Joanita Joseph -TMC


Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Mheshimiwa Abdallah Mtinika ametoa wito kwa wananchi kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi na ushuru stahiki ili kuwezesha Manispaa na Serikali kwa ujumla kupata mapato kwa ajili ya kupanga mikakati ya kuwaletea maendeleo.


Mheshimiwa Meya ametoa wito huo leo Septemba 27, 2023 kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelezea mafanikio yaliyopatikana kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ulioishia tarehe 30 Juni 2023.


Mhe. Mtinika amesema kuwa Halmashauri kwa mwaka huo wa fedha imefanikiwa kukusanya Tshs Bilioni 43.9 kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ya ndani ikiwa sawa na asilimia 101 ya lengo la makusanyo na Tshs Bilioni 19.9 kutoka humo zimetumika kutekeleza miradi ya maendeleo.


"Kwa mwaka huu mpya wa fedha 2023/2024 kiasi kilichopangwa kukusanywa ni Tshs Bilioni 47.7, hivyo niwaombe wananchi tulipe kodi, wenye malimbikizo ya madeni walipe lakini pia tumejipanga kudhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato ikiwemo kupokea taarifa ya vyanzo vinavyopotea ili kuzuia uvujaji wa fedha za halmashauri" alisema Mhe. Mtinika.


Vilevile ameeleza kuwa halmashauri ilipokea ruzuku kutoka serikali kuu ya Tshs Bilioni 10.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule mpya za msingi na sekondari, ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na uboreshaji katika sekta ya afya.


Halikadhalika ameeleza kuwa halmashauri ilifanikiwa kutenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya utoaji mikopo kwa wanawake , vijana na walemavu ambapo kiasi cha Tshs Bilioni 2.9 kimetumika kwa makundi hayo.


Amehitimisha mkutano huo kwa kusisitiza wananchi kuendelea kutunza amani iliyopo nchini na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Menejimenti na watendaji wote wa Halmashauri ya Temeke kwa kuwezesha mafanikio hayo.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke