• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Mstahiki Meya awaondoa hofu wakazi wa Kata ya Kijichi

Posted on: December 11th, 2019

 “HATUJAGAWA KIZIMBA HATA KIMOJA SOKO LA KIJICHI WANANCHI WA KIJICHI ONDOENI HOFU” MHE.CHAUREMBO.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Mhe Abdalah Chaurembo amewahakikishia wananchi wa kijichi kuwa bado vizimba vya soko la Kijichi havijagawiwa kwa wanachi kinachofanyika sasa wananchi wanachukua fomu za kuomba kupatiwa vizimba.

Na mchakato wa kugawa vizimba katika soko hilo lazima maamuzi yafanyike kupitia Kamati ya Fedha na  Baraza la Madiwani ambapo Mhe Diwani wa Kata hiyo atashiriki kikamilifu kwa kuwa yeye ndiye Mwakilishi wa wananchi katika eneo hilo.

Ametoa ufafanuzi huo jana ofisini kwake Manispaa ya Temeke Makao Makuu wakati akifanya mahojiano na TMC TV kufuatia minong’ono iliyoanza kuenea kwa wananchi kuwa Manispaa ya Temeke imeshaanza kugawa vizimba katika Soko la Kijichi.

Mhe Abdalah Chaurembo amesema mnamo tarehe 21 Octoba 2019 Menejimenti ya Halmashauri ya  Manispaa Temeke katika kikao cha kamati ya fedha  ilileta agenda mbalimbali miongoni mwa agenda hizo agenda namba 7 ilikuwa ni kuwasilisha mapendekezo ya rasimu ya muongozo wa uendeshaji wa masoko na vituo vya daladala.

“Katika kujadili ajenda hizo tuliweza kuzungumza mambo mbalimbali na mojawapo ni namna gani tunaweza kugawa vizimba na maduka katika masoko yetu tuliyo yaboresha. Nikisoma katika rasimu imeelekeza kuwa katika ugawaji wa vizimba hivyo wafanya biashara watapata miezi mitatu ya matazamio katika miezi hiyo watafanya biashara bila kulipa chochote yaani “Grace Period” na hiyo itahusisha wafanyabiashara wapya tu ambao wapo awali hawakuwa na vizimba pia kipaumbele kitakuwa kwa wafanyabiashara wa zamani katika eneo husika” Alisema Mh. Chaurembo

Aidha Mhe Chaurembo alisisitiza kuwa katika masoko yote yaliyoboreshwa katika Manispaa ya Temeke ugawaji wa vizimba kipaumbele kikubwa kitakuwa ni kwa wenyenyeji wa maeneneo husika yaani wale ambao awali walikuwa wanafanya biashara katika maeneo hayo na wakapisha ujenzi huo wa soko na wale ambao ni wazawa yawezekana awali hawakuwa wakifanya biashara lakini sasa wanataka kufanya biashara na wananchi wa kata za jirani zilizopo ndani ya wilaya ya Temeke.

Ifahamike kuwa Soko la Kijichi ni miongoni mwa masoko ya kisasa ambayo yamejengwa na Mradi wa DMDP katika halmashauri ya Manispaa ya Temeke na yana sehemu nzuri za maduka pamoja na vizimba na hiyo yote ni katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi  na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU  kama Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli anavyoisimamia kuhakikisha wanachi hasa wa kipato cha chini wanakuza vipato vyao.

Katika picha ni mwonekano wa vizimba kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo katika soko la kisasa kijichi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke