• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

NJOMBE MJI NA ILALA WAPATIWA DARASA TEMEKE LA UENDESHAJI MASOKO MAPYA YA KISASA.

Posted on: November 27th, 2020

Halmashauri ya Mji Njombe pamoja na Manispaa ya Ilala wamefanya ziara ya mafunzo ya kimkakati katika Manispaa ya Temeke kujifunza namna bora ya uendeshaji wa masoko mapya ya kisasa.

Wataam hao wamezuru Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam mapema leo na kupokelewa na Mkurugenzi wa Manispaa Ndg Lusubilo Mwakabibi akiwa na timu ya wakuu wa Idara na vitengo wa Manispaa, kisha kupata wasaa wa kubadilishana uzoefu wa namna taasisi hizo zinavyoweza kufanya vizuri katika nyanja za masoko kwa lengo la kuleta ustawi wa jamii za kitanzania.

Akiongea wakati wa ziara ya kutembelea baadhi ya masoko mapya ya kisasa yaliyojengwa na Manispaa ya Temeke kupitia mradi wa DMDP ‘Dar es Salaam Metropolitan Development Project’ Katibu tawala wa Mji wa Njombe Ndg. Emmanuel George amesema Njombe Mji wanatekeleza mradi mkubwa wa Soko la kisasa katikati ya Mji, kwa sasa Soko hilo limekamilika kilichobaki ni wafanyabiashara kuanza kulitumia  Soko hilo.

Kwa kuwa Temeke inauzoefu katika uendeshaji wa masoko mapya wakaona ipo sababu ya kufanya ziara ya kimkakati kujifunza namna Temeke ilivyofanikiwa na changamoto inazopitia katika uendeshaji wa masoko kwa ujumla wake.

Vilevile kuweza kuzitangaza fursa zinazopatikana katika Mji wa Njombe kwa mfano kilimo cha Parachichi ambacho sasa kina Soko kubwa ndani na  nje ya nchi pamoja nakuona uwezekano wa wafanyabiashara wa Njombe na Temeke kufanya biashara kwa pamoja kama kuleta viazi katika masoko ya Temeke na bidhaa zingine zinazofanana na hizo.

Kwa upande wa mratibu wa mradi wa DMDP Temeke Ndg Edward S.Haule amesema kinachofanyika Temeke ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kupitia Ilani ya CCM yenye lengo la kuwainua wananchi au kuleta ustawi katika Maisha ya kila siku, wageni kutoka Njombe na Ilala wamekuja kujifunza na kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kuendesha masoko mapya.

Kupitia masoko 2 waliyotembelea Kijichi na Makangarawe wameweza kujifunza muundo wa usimamizi wa masoko, usafi na utunzaji wa miundombinu ya soko, namna masoko yanavyoweza kuwa vyanzo vya mapato pia Temeke inavyoweza kufanya kazi kwa timu kwa kuwa suala la masoko ni mtambuka linahitaji ushikiano wa Idara na vitengo vyote.

“Aidha ujio wa wageni wanaokuja kujifunza au kupata uzoefu Temeke wanatupa morali ya kuongeza juhudi ili kuweza kufanya vizuri zaidi ya hapa tulipo” alisema Ndg Edward.

Mwisho Mkurugenzi wa Manispaa amefafanua kuwa Manispaa ya Temeke imekuwa ikipokea wageni kutoka mikoa na Halmashauri mbalimbali Nchini wakija kujifunza utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hiyo ni faraja kwetu lakini pia inatuongezea nguvu ya kukimbia zaidi kwa kuwa wabunifu katika kuibua miradi na utekelezaji wake ili kuleta ustawi wa wananchi.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke