• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

SAA 48 TU ZATOSHA KUTIMIZA AGIZO LA DC JOKATE

Posted on: September 4th, 2021

Kufuatia ziara aliyoifanya Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Jokate Mwegelo siku ya Ijumaa tarehe 03/09/2021 na kuagiza kuwekwa kwa matuta ya barabarani eneo la Mzinga -Kongowe katika Manispaa ya Temeke mara baada ya mwanafunzi mmoja kugongwa na gari,agizo hilo limetekelezwa  ndani ya siku mbili(saa 48).


Akiwa katika eneo hilo leo Jumatatu alipokwenda kukagua utekelezaji huo,Mhe.Jokate aliwataka madereva kuzingatia sheria na alama za barabarani huku akiwataka wanafunzi na watumiaji wengine kuwa makini wanapovuka barabara.


"Sisi tutafanya jitihada kama Serikali kuhakikisha usalama wenu unakuwepo lakini pia jitihada za mtu mmoja mmoja ni muhimu sana".Mhe Jokate alisema


Naye kamanda wa Polisi wa wilaya ya kipolisi Mbagala Joseph Mwakabonga alisema kuwa jeshi la Polisi litahakikisha linawashughulikia madereva wote ambao hawatafuata sheria za barabarani ili kuweza kupunguza ajali katika maeneo hayo na mengine ndani ya Wilaya hiyo.


''Nitahakikisha vijana wangu wanakuwepo barabarani kusimamia agizo la Mkuu wa Wilaya lakni uwepo wao pia uambatane na kutii sheria za barabarani kwa madereva".Alisisitiza Kamanda huyo.


Mwalimu Sabia Mwantobe wa Shule ya Msingi Mzinga alimueleza mwandishi wa TMC Tv kuwa takribani wanafunzi 8 wameshagongwa na magari katika eneo hilo na kuwepo kwa matuta kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa ajali huku akimshukuru Mkuu wa wilaya huyo kwa kulipa uzito jambo hilo.


"Imekuwa faraja kwetu na kwa jamii pia,tunashukuru ujio wa Mkuu wa wilaya kumefanya uwekaji wa matuta kwa haraka sana....huyu mtoto wa juzi aligongwa nimeshuhudia,ilikuwa mbaya sana".Alidai Mwl.Mwantobe


Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es salaam Elson Mwelasi aliwashauri maderava kutii alama na sheria za barabarani ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukwa endapo sheria zikifuatwa.


Hivi karibuni wanafunzi wa shule hizo walilazimika kufunga barabara kwa muda katika eneo hilo wakishinikiza kuwekwa kwa matuta mara baada ya mwanafunzi mwenzao kugongwa na gari hali iliyosababisha jeshi la polisi kuingilia kati kuwatawanya na kupelekea Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Jokate kufika eneo hilo na kutoa maagizo kadhaa kwa Wakala wa barabara nchini(TANROADS) ikiwemo kuwekwa kwa alama za barabarani.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke