• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

TEMEKE KUWA NA MAHAKAMA YA MFANO NCHINI

Posted on: August 5th, 2021

                      

Katika kuhakikisha kunakuwa na uharakishwaji wa uendeshwaji wa kesi zinazohusu mirathi, talaka na zile zinazohusu watoto. Serikali inakamilisha ujenzi wa jengo la kisasa la mahakama katika eneo la Chang’ombe wilayani Temeke litakalokuwa maalumu kwa kuendeshea mashauri hayo.

Akikagua jengo hilo leo Alhamisi tarehe 05.08.2021,Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Jokate Mwegelo amesema kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutakuwa ni suluhisho kwa mashauri hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakicheleweshwa kutokana na Mahakama nyingi kuwa na mashauri mengine tofauti.

‘’Takwimu zinaonesha kuwa wilaya yetu ina idadi kubwa sana ya watu na kuna wastani wa watoto zaidi ya 100 wanaozaliwa kila siku. Hii inapelekea kuwa na migogoro na kesi nyingi za mirathi, kesi za watoto na hata talaka’’.Alisema Mhe.Jokate

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu wilaya ya Temeke Mhe.Ilvin Mugeta,alisema ujenzi wa Mahakama hiyo utasaidia kupunguza muda wa kumaliza shauri kutoka miaka mitatu hadi mitano ya sasa mpaka miezi sita  huku akisisitiza wananchi kuitumia miundo mbinu ya Mahakama hiyo vizuri.

Aidha wabunge wa majimbo ya Temeke na Mbagala ambao walikuwa miongoni mwa walioambatana na Mkuu wa Wilaya kutembelea jengo hilo na kukagua,walimshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa wanawake pamoja na watoto ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa ndio waathirika wakuu katika masuala ya mirathi.

“Niwaombe tu wananchi waweze kuitunza mahakama hii ili iweze kudumu kwa kuwa uwekezaji huu wa serikali ni mkubwa kwa hiyo hatuna budi kudumisha usafi na kutunza mazingira yake kwa kuwa Mahakama hii ni ya mfano hapa Dar es salaam na nchi nzima’’.Alishauri Mbunge wa Mbagala Mhe.Abdallah Chaurembo

Awali akitoa maelekezo kwa Mkuu wa wilaya Msanifu majengo wa jengo hilo,Kailat Bakar alisema jengo hilo limekidhi mahitaji yote ikiwemo mahabusu za watoto,wanawake,wanaume pamoja na sehemu maalumu ya kinamama kunyonyesha watoto wanapokuwa wakiendelea kusikiliza kesi zao.

Jengo hilo litakuwa la kwanza la aina yake hapa nchini ambapo kutakuwa na mahakama ya mwanzo, wilaya na mahakama kuu ambapo zitakuwa ni maalumu kwa kusikiliza mashauri yanayohusu kesi za mirathi, talaka na watoto na linatarajiwa kufunguliwa rasmi mwezi wa tisa mwaka huu na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke