• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

‘‘Temeke Tunazungumzia Viwango Vingine’’Mkurugenzi .

Posted on: August 8th, 2019


Mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Temeke ndugu Lusubilo Mwakabibi ametoa rai kwa halmashauri nyingine  kufika, kuona na kujifunza teknologia inayopatikana ndani ya banda la manispaa ya Temeke.Ndugu Lusubilo ametoa rai hiyo jana  mara baada ya kutembea na kujionea mambo mbalimbali yanayofanyika katika banda la halmashauri yake.

Akizungumza katika mahojiano mafupi  Mwakabibi amesema “Temeke tumeingia katika mazingira ambayo ni ya kiwango kingine cha kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania za kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa nchi ya viwanda.Tumewawezesha wajasiliamali wetu,sasa wanafanya vitu vikubwa.Halmashauri nyingine zimefanya mambo mazuri,lakini Temeke tumefanya kwa viwango vya juu.Karibu Temeke ujifunze na uone mambo makubwa.Sio kwamba ununue tu,lakini uchukue teknolojia tuliyonayo ,upeleke kwenye halmashauri yako’’.

Mwakabibi  ameonyesha kuridhishwa na kiwango cha ubora wa bidhaa za wajasiliamali ambapo  amesema kwamba wamefanya vizuri kwenye eneo la viwanda vidogo  vidogo, wanasindikika bidhaa za aina mbalimbali ,ufungashaji  wao pia ni mzuri sana kiasi ambacho mtu anapoziona anaweza kufikiri kwamba bidhaa hizo zimetoka katika nchi zilizoendelea.

Kadhalika Mwakabibi amesema kwamba  Temeke sasa wameingia katika eneo la viwanda ambapo katika banda la manispaa ya Temeke kipo kiwanda cha kutengeneza viatu  ambacho  wanauwezo wa kumpima mtu kiatu,kumtengenezea na akaondoka na viatu vyake vikiwa vimekamilika, jambo ambalo linaonyesha kwamba Temeke iko kwenye kiwango kingine.

Mwakabibi ameendelea kusema kwamba  ,wanataka viatu vinavyozalishwa na kiwanda hicho, visiishie  kuuzwa Temeke tu ,bali wanataka viende nje ya Tanzania.Amesema kama ambavyo Mhe. Rais ametangaza kwamba mkutano wa SADEC unafanyika hapa Tanzania, nchi 16 zitakuwepo hapa nchini kuanzia tarehe tisa,na tarehe 17 na 18 Marais wa nchi zote 16 watakuwepo,Temeke watatumia fursa hiyo kuhakikisha kwamba watakaokuja kwenye mkutano huo wanaondoka na viatu vinavyotengenezwa na kiwanda hicho  ,ili soko lake liweze kukua.

Halmashauri ya manispaa ya Temeke  imekuwa ikitumia asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi, ambapo katika siku za hivi karibuni mkazo umewekwa zaidi kwenye kuwapatia vitendea kazi.Kwa mtindo huo walengwa hao wameweza kujiunga katika vikundi ambapo vitendea kazi hivyo hupelekwa kwenye vikundi hivyo,kwa kuzingatia mahitaji  ambayo kila kikundi kimeyaainisha.Kupitia uwezeshaji huo, kiwanda cha kufyatua tofali, kiwanda cha viatu vimeweza kuanzishwa,na vingine vingi viko mbioni kuanzishwa.



........... MWISHO.........


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke