• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Temeke Yapokea Ugeni wa Nchi Tano

Posted on: November 17th, 2021

Novemba 15,2021 Meya wa manispaa ya Temeke  Mheshimiwa Abdallah Mtinika kwa kushirikiana na mkurugenzi wa Manispaa ndugu Elihuruma Mabelya  walipokea  ugeni kutoka nchi tano (5)  ambazo ni Swideni,Uganda,Kenya,Zambia na Tanzania.

Lengo la ugeni huo likiwa ni kuzungumzia mpango wa muda mrefu juu ya masuala ya kijinsia, kupitia programu inayozishirikisha Manispaa ,programu  ambayo inafadhiliwa na   shirika lisilo la faida la ‘Swedish International Centre for Local Democracy’ (ICLD).

Akizungumza  wakati wa kikao hicho  kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa( Idd Nyundo) Mhe. Mtinika alisema“Manispaa ya Temeke imeshiriki katika maswala haya ya kijinsia ambayo yanahusisha nchi mbalimbali,kama halmashauri  hatupo nyuma kwenye kuhakikisha tunakwenda sambamba na malengo ya kidunia ya mwaka 2020-2030 ili tuwe tuwe sawasawa na wenzetu, waliokuja kujifunza Temeke wamepongeza hatua tulizopiga katika eneo hilo na tunaamini tutaendelea kufanya vizuri.

Tutambue kwamba dunia ni kijiji na inayo malengo ,kuna malengo 17 yanayotakiwa yafuatwe ili tuwe na dunia endelevu, kati ya hayo ni hili la usawa wa kijinsia (lengo namba 5) nasi kama sehemu ya dunia tuendelee kutimiza na kufuata haki za watoto wa kike na kina mama ili mambo ya usawa wa kijinsia yawe sawa”.

Katika kikao hicho ambacho kilichojumuisha wageni hao, wakuu wa idara mbalimbali pamoja na vijana wa kike ambao wamewezeshwa kiuchumi kupitia mikopo inayotolewa na Manispaa pamoja na ruzuku zinazotolewa na Serikali kupitia mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF). ,katibu mkuu wa ICLD  ndugu Johan Lilja alisema ‘’Kitu  kimoja ambacho nimegundua ni kwamba unapompa mwanamke jukumu, vitendo vinatokea.nimeona  leo, timu yangu (Anne  na Annamaria),sijahusika kufanya chochote, lakini mmejionea wenyewe.tuwaruhusu wale wasichana ambao ni imara kupata nafasi .

kitu cha pili ninachotaka kusema ni kuwatia  moyo  ninyi  nyote ,unajua linapokuja suala la maendeleo , wanaume wakati mwingine wanaonekana kuogopa, wanataka kujikita kwenye vile vitu walivyonavyo.lakini nawaambia kwa uzoefu nilionao wa zaidi ya miaka 30, najua, nina uthibitisho,nina ushahidi kwamba  ukiruhusu hicho kidogo , huku ukiwahusisha wanawake,kinakuwa kikubwa.na kuwa na 50% ya kitu ambacho ni kikubwa ni mantiki zaidi kuliko kuwa na 100% ya kitu kidogo’’.Hivyo kwa kuwashirikisha wanawake, tunafanya kwa jamii ,kwa Manispaa, kwa Nchi na kwa Dunia.unataka kuwa  chanzo cha mabadiliko, unayo fursa, kama hukufanya kabla, anza leo’’.


ICLD ni shirika lisilo la faida linalofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Swideni (SIDA).Dhima ya shirika hilo ni kusaidia jamii katika masuala ya  demokrasia,mabadiliko na ugatuzi wa madaraka katika ngazi ya mamlaka za serikali za mitaa, kwa kuwawezesha watendaji wa mamlaka hizo kufanya tafiti katika maeneo ya usawa wa kijinsia ,ushirikishwaji, uwazi na uwajibikaji kwa lengo la kuleta maendeleo katika mamlaka hizo.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke