• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

"TUTAHESHIMU MAAMUZI YA MAHAKAMA" DC TEMEKE.

Posted on: December 4th, 2020

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Godwin Gondwe, amewahakikishia Wanachi wa kata ya Yombo Vituka mtaa wa Magogoni kwamba , wao kama serikali ya Wilaya,wataheshimu maamuzi yatakayotolewa na Mahakama, baada ya kumalizika kwa kesi iliyofunguliwa na Wakazi 56 wa eneo hilo, kufuatia mgogo wa ardhi uliopo baina yao na halmashauri ya Manispaa ya Temeke.

Mhe. Gondwe ametoa kauli hiyo leo asubuhi, wakati wa kikao chake na Wananachi pamoja na Viongozi wa eneo hilo.Kikao ambacho kimefanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Lumo.

Akizungumza mara baada ya kuwasikiliza Wananchi wa eneo hilo, Mhe. Gondwe amesema " Mlimuomba Mheshimiwa Rais aje kuwasikiliza,mimi ni muwakilishi wa Mhe. Rais,nimekuja kuwasikiliza,mgogoro huu haujatushinda, tutaumaliza kwa amani na kila mtu atafurahi.

Maelekezo ya Serikali ni haya; Kwanza itisheni Mkutano Mkuu, Diwani Mteule mara baada ya kuapishwa,shirikiana na Mtendaji wa Kata,muitishe Mkutano Mkuu, mkae kwa pamoja muutambue mgogoro huu,na mukhtasari uandikwe.Mgogoro huu ni wa muda mrefu, unapaswa kutambuliwa kupitia vikao halali vya Kata.

 Baada ya kuutambua ,kwa sababu kesi inayohusu mgogoro huu iko Mahakamani, Wananchi mnaohusika, mhudhurie Mahakamani,kesi ifike mwisho, mgogoro huu uishe. Wanasheria wetu watawasaidia kulifuatilia hili,msije mkawa mnawanufaisha watu wachache.Inawezekana mgogoro huu umeendelea kuwepo kwa muda mrefu, kwa sababu kuna watu wananufaika.Miaka 22 ni mingi sana jamani,kuna watu wamezaliwa wameukuta huu mgogoro,wengine wamekufa wameuacha.Mgogoro huu uishe.

Pili,nasitisha ujenzi katika eneo hili mpaka Mahakama itakapotoa maamuzi. Sisi tutaheshimu maamuzi ya Mahakama,na baada ya maamuzi , muitishe tena Mkutano Mkuu, mjadiliane kwa pamoja,Wananchi wote wafahamu maamuzi yaliyotolewa,baada ya kuyafahamu ,mtafanya maamuzi ya pamoja, kutokana na Mahakama itakavyokuwa imeamua.Mimi nitaleta wataalamu wangu wa Ardhi,watakuja kuwashauri."

Kwa upande wao Wananchi ,wameonyesha kuridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya,ambapo wamesema kwamba wanamshukuru sana kwa kufika katika eneo hilo,na kwamba wanaamini kuwa haki itatendeka.

Aidha Mhe. Gondwe amesema kwamba wao kama Serikali nia yao ilikuwa njema kabisa,ambapo  kutokana na uhitaji wa dharura wa madarasa, kwa ajili ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2021 ,waliamua kulitumia eneo hilo, kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 6 ili kuwawezesha watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo, kupata mahali pa kusomea.Lakini kwa sababu ya mgogoro huo,mradi huo wa ujenzi wa madarasa, utapelekwa katika shule nyingine.

Katika hatua nyingine Mhe. Gondwe ameielekeza idara ya  Mipango Miji manispaa ya Temeke, kutambua mipaka ya maeneo yote ya shule zote za msingi  na  Sekondari,na kuweka alama kwenye mipaka ya maeneo hayo, ili kuzuia uvamizi, na kuepusha migogoro ambayo, baadhi ya watu wamekuwa wakiisababisha, kwa lengo la kujinufaisha.

Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na daktari John Pombe Joseph Magufuli inatekeleza sera ya elimu bila malipo.Moja wapo ya mafaniko makubwa katika utekelezaji wa sera hiyo, ni ongezeko kubwa la uandikishwaji wa watoto wanoingia darasa la kwanza, sambamba na ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba.

Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa ongezeko kubwa la uhitaji  wa  miundo mbinu mashuleni ,hususani madarasa kila mwaka, ili kukidhi idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza,na wanaojiunga na kidato cha kwanza.

Kufuatia uhitaji huo, Manispaa imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuhahakisha kwamba hakuna mtoto anaechaguliwa ama anaeandikishwa, anakosa pa kusomea,ambapo ndani ya mwaka 1, imefanikiwa kujenga madarasa 120,pamoja na matundu ya vyoo 124 ,na katika jitihada hizo hizo imepanga kujenga vyumba vingine 54, na tayari utekelezaji  umeanza.Katika shule mbali mbali za sekondari  ujenzi unaendelea, ifikapo Januari 11, 2021,asiwepo  mwanafunzi aliyechaguliwa atakaebaki.

Na kwa kuwa nia ya Manispaa ni njema,ni vema jamii yote ikaiona nia hiyo njema, na kuunga mkono jitihada hizo, ili kuendelea kulisukuma mbele gurudumu la elimu kwa manufaa ya watoto wetu waliopo sasa,na vizazi vijavyo.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke