• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

"UKWEPAJI KODI NA UCHAFUZI WA MAZINGIRA SASA UWE HISTORIA" MKURUGENZI MWAKABIBI.

Posted on: January 27th, 2021

Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke Ndg Lusubilo Mwakabibi ametangaza kiama kwa wale wote wanaokwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali zinazotozwa na Manispaa pamoja na uchafuzi wa mazingira katika maeneo yote ya Manispaa.

Ameyasema hayo leo wakati akiongaea na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa makao makuu Jijini Dar es salaam.

Akiongea juu ya uchafuzi wa mazingira Bwana Mwakabibi ameonyesha kukerwa na uchafu katika miundo mbinu ya barabara ambayo serikali imetumia gharama kubwa kuijenga na kwa bahati nzuri kwa sasa Temeke imezungukwa na barabara za lami hadi mitaani tena barabara hizo zina taa na zinavutia.

"Ni kwa nini sasa mwananchi wa Temeke au kutoka sehemu nyingine atupe taka ovyo au haoni umuhimu wa kufanya usafi katika eneo lake hali hiyo kwa Temeke haivumiliki" alisema Mwakabibi.

Mkurugenzi wa Manispaa Ndg Lusubilo Mwakabibi akitoa maagizo kwa wananchi wa Temeke kupitia  vyombo vya habari katika ukumbi wa Manispaa (Iddy Nyundo)


Ameweka bayana kwamba sheria zipo wazi, mfano sheria ya mazingira ya mwaka 2004 sura namba 288 kifungu 89 inayohusu sheria ya udhibiti wa uchafuzi wa mazingira imetamka mtu yeyote atakayekiuka ametenda kosa, na iwapo atapatikana na hatia,adhabu kali itatolewa dhidi yake ikiwemo kulipa faini ya Tsh 50,000/= au kifungu kisichopungua miezi 12 jela au vyote kwa pamoja.

Sambamba na hilo kwa upande wa wakwepa kodi na tozo mbalimbali zinazotozwa na Halmashauri hawavulimiki tena, ifahamike kuwa maendeleo yoyote yanayofanyika katika Manispaa yanatokana na kodi ambazo mwanatemeke anatakiwa kulipa.

Mfano mzuri hivi sasa Manispaa ya Temeke inajenga vyumba vya madarasa zaidi 91 fedha za utekelezaji wa ujenzi huo ni kutoka katika makusanyo ya ndani ambapo upatikanaji wa mapato hayo ni lazima kodi zilipwe.

Aidha Mkurugenzi wa Manispaa ametoa rai kwa wale wote wanaofanya biashara Temeke iwe ni  kwenye kizimba, maduka ya jumla na rejareja kuhakikisha wanalipa kodi na tozo zingine zinazotozwa na Manispaa.

''Kwa ujumla katika suala la usafi na ulipaji kodi kuanzia sasa iwe namba moja kwa kila mtu ndani Manispaa ya Temeke  kama kauli yetu inayotumika siku zote ya "Temeke ya Viwango" na Manispaa imejipanga vizuri''.Alisisitiza  Mwakabibi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke