• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

UWEKEZAJI BANDARI YA DAR ES SALAAM KUNUFAISHA WENYE BANDARI KAVU (ICD)

Posted on: August 4th, 2023

Na: Joanita Joseph

Mkuu wa Wilaya ya Temeke. Mheshimiwa Mobhare Matinyi, tarehe 03/08/2023 alifanya ziara ya kukagua shehena inayohudumiwa na bandari kavu (Inland Container Depot - ICD) ya Harpended Explorer Scout Unit (HESU) iliyopo katika kata ya Miburani, wilayani Temeke.


Katika ziara hiyo aliambatana na mbunge wa jimbo la Temeke Mhe. Dorothy Kilave, Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke Nicodemas Tambo, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Temeke, George Sayi, pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Miburani, Abeid Mvuma.


Akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya alisisitiza ushirikiano baina ya serikali na wawekezaji kwani uwekezaji unaotarajiwa kufanywa utaboresha zaidi bandari ya Dar es salaam na kuiwezesha kuhudumia takribani tani milioni 38 za mizigo ifikapo mwaka 2030.


"Ubora wa huduma ya bandari hii umetokana na uamuzi wa Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kununua mitambo mitatu ya kupakua na kupakia makasha ya mizigo (Ship to Shore Gantry - SSG) ambapo mmoja una thamani ya shilingi za Tanzania bilioni 40 hadi 50.


Mhe. Matinyi alieleza kuwa uwekezaji huu utasaidia kuhudumia nchi jirani kwa ukamilifu akizitaja Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Zambia, Malawi, Zimbabwe na hivi sasa hata Msumbiji, Komoro isiyokuwa na bandari kubwa na Sudan Kusini.Mhe. Matinyi alisema nchi hizo kwa mwaka zina shehena ya jumla ya zaidi ya tani milioni 70. Hivi sasa sehemu ya shehena hii inahudumiwa na bandari za Mombasa, Beira, Maputo, Walvis Bay na Durban.

Kati ya tani milioni 21.27 ambazo bandari ya Dar es Salaam ilizihudumia mwaka 2022/23 ni tani milioni 8.5 tu ndizo zilizotoka katika nchi hizi.

"Mipango ya baadaye ya bandari ni kuboresha magati namba 8 hadi 11; kuhamisha kituo cha kupokelea mafuta na gesi kutoka Kurasini kwenda Kigamboni pamoja na kuongeza magati namba 12 hadi 15.

Awali serikali ilishatumia jumla ya dola za Marekani milioni 420 kujenga yadi namba 5 hadi 7 zenye uwezo wa kutunza makasha 10,000; kutanua na kuongeza kina cha mlango bahari wa kuingilia bandarini, kujenga gati namba 0 lenye urefu wa mita 320 na eneo la kutunza magari 6,000; kuongeza kina cha magati namba 1 hadi 7 kutoka mita 7 hadi 14.5 pamoja na upana wake kwa mita 15.

Mhe.Matinyi amefanya ziara hii ikiwa ni moja kati ya malengo yake ya kutembelea maeneo yote yanayojishughulisha na shughuli za kiuchumi wilayani Temeke.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke