• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

WAFANYAKAZI KIWANDA CHA NONDO MBAGALA WALIA NA MAZINGIRA MAGUMU YA KAZI

Posted on: December 21st, 2022

Na:Shalua Mpanda-TMC

Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza nondo cha A.M Steel & Iron Mills kilichopo Mbagala wilayani Temeke wamelalamika kutokuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi.


Wakizungumza na Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke ndugu Elihuruma Mabelya ambaye aliambatana na Mstahiki meya wa manispaa hii Mhe.Abdallah Mtinika wakati wa ziara ya kushtukiza walioifanya kiwandani hapo leo,wamesema mazingira wanayofanyia kazi ni hatarishi.


Mmoja wa wafanyakazi kiwandani hapo amewaeleza viongozi hao kuwa sehemu kubwa ya kazi zinazofanywa kiwandani hapo hutumia moto mkali lakini hawana vifaa vya kuwakinga na joto hilo kali hali inayoweza kuhatarisha afya zao.


Akizungumza mara baada ya kukagua kiwanda hicho,Mstahiki meya Mtinika ameonesha kusikitishwa na mazingira ya kazi katika kiwanda hicho na kuelekeza mamlaka husika kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa ili kuokoa maisha ya wafanyakazi hao.


" Leo tumekuja hapa baada ya kupata malalamiko ya muda mrefu,kwa kweli tuliyoyakuta ni mambo ya hatari,mazingira ya kazi si mazuri hata ukitazama wafanyakazi hawana vitendea kazi wanavaa kandambili,hii hali imenisikitisha".Alisema Mhe.Mtinika.


Naye mkurugenzi wa manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya amesema kiwanda hicho kimekiuka taratibu za uendeshaji huku akisisitiza kuwa Serikali inapenda uwekezaji kwa kuwa unawezesha kukusanya kodi lakini kodi hiyo isitoke kwenye mazingira yanayoumiza wananchi.


Mbali na mazingira yasiyo rafiki kwa wafanyakazi, Viongozi hao wamebaini uharibifu na uchafuzi wa Mazingira kiwandani hapo ambapo moshi unaotokana na shughuli za uzalishaji wa nondo umekuwa ukitoka nje na kuathiri wanaozunguka eneo hilo.


Licha ya kazi zinazofanyika kiwandani hapo kutumia kiwango kikubwa cha moto lakini wafanyakazi wa kiwanda hicho wamekutwa wakifanya kazi zao bila kuwa na kinga za mikono(gloves),viatu vigumu wala kofia ngumu.


Ziara hiyo ambayo iliwajumuisha wataalamu wa mazingira kutoka Manispaa ni matokeo ya kauli ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwataka viongozi kwenda kutatua kero na changamoto za Wananchi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke