• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

''Watanzania Waje Waone Maajabu Temeke'' DC

Posted on: August 7th, 2019


Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Felix  Lyaniva ametoa wito kwa wakazi wa manispaa ya Morogoro na Watanzania kwa ujumla  kufika katika banda la halmashauri ya manispaa ya Temeke ili waweze kujionea mambo mazuri yaliyopo pamoja na kupata elimu katika kilimo,Mali asili, mifugo na uvuvi.Mhe. Lyaniva ametoa wito huo  mapema leo alipotembelea banda la Halmashauri ya manispaa ya Temeke  lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya Nanenane Morogoro.

Akizungumza mara baada ya kutembea ndani na nje ya banda la Manispaa ya Temeke Mhe. Lyaniva amesema ‘‘Nimefika, nimetembea,nimeona mambo mazuri sana, Nimeona kiwanda cha kutengeneza viatu, unapima kiatu hapohapo,unatengenezewa unaondoka nacho.Kuna mimea ya aina mbalimbali hapa,kuna clinik ya mimea ,kuna bwawa la samaki , kuna mizinga ya nyuki,kuna asali ,kuna masega ya asali, kuna mtego  kwa ajili ya kuangamiza kunguru weusi,kuna wanyama wa aina mbalimbali,hata mbwa yupo hapa, kuna bidhaa mbalimbali za kusindikwa, kuna mapambo ya kina mama,viatu,mikoba,nguo.Hapa ni mahali pazuri sana pa kujifunza.Njoo ufundishwe jinsi ya kulima kilimo kitakachokunufaisha,njoo ufundishwe jinsi mbwa anavyoweza kukusaidia kulinda mazao yako shambani ,njoo ufundishwe namna unavyoweza kufuga samaki na kujipatia kipato, njoo ujifundishwe namna bora ya kufuga nyuki, na jinsi ya kurina asali,njoo ujifunze kwa wajasiliamali wetu, na wewe uweze kutoka kimaisha.Nachukua fursa hii kuwakaribisha wakazi wa manispaa ya  Morogoro na Watanzania wote  waje waone maajabu  Temeke’’.

Mhe. Lyaniva pia amesema kwamba Temeke imejipanga vema,kwani hata bidhaa za wajasiliamali wake ni za kiwango cha juu  , hali inayodhihirisha kwamba wana Temeke wamedhamiria kuunga mkono kwa vitendo kauli mbiu ya Mhe. Rais ya kuwa na Tanzania ya viwanda.

Aidha  amewataka Watanzania ambao ni walengwa wa TASAF kufika katika banda la manispaa ya Temeke ili waone jinsi ambavyo walengwa wa TASAF Temeke wanavyotumia fedha za ruzuku  kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.Wamejiunga kwenye vikundi, wamejifunza kutengeneza vitu mbalimbali,wanajipatia kipato.Katika hatua nyingine  Mhe. Lyaniva  amewapongeza wataalamu wa halmashauri ya manispaa ya Temeke waliohusika katika maandalizi ya nanenane kwa mwaka 2019 kwa namna ambavyo wamefanya maandalizi mazuri, na kila mwaka wamekuwa wakiboresha ili kuhakikisha kwamba mambo yanakwenda vizuri..

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kama zilivyo halmashauri nyingine inashiriki katika maonesho ya wakulima na wafugaji – nanenane kanda ya mashariki ,ambapo vitu vyote vinavyoonyeshwa katika banda lake  viko katika ubora wa kiwango cha juu.



..........MWISHO...........

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke