• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 100 ZATUMIKA KUTEKELEZA AFUA ZA LISHE TEMEKE

Posted on: May 23rd, 2024

Na:Francisca Mselemu

Kamati ya lishe Manispaa ya Temeke imekaa kikao chake cha robo ya tatu Mei 23,2024 ambapo kikao hicho kimehusisha uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kutoka divisheni za Elimu Msingi,Elimu Sekondari,Maendeleo ya Jamii pamoja na Kilimo,Mifugo na Umwagiliaji.


Akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe, Mratibu wa lishe manispaa ya Temeke Bi. Happy Mkunda amesema kuwa kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024 Manispaa imetumia asilimia 119.99 sawa na shilingi 106,773,076.00 ya fedha zilizopangwa kutekeleza afua za lishe kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato.


Akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha hizo Bi Mkunda amesema:


‘‘Manispaa imetoa fedha kwa wakati,utolewaji wa fedha hizo umewezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe zikiwemo kutenga zaidi ya shilingi 1000 kwa kila mtoto,ambapo tuliweza kutenga kiasi cha shilingi 2,526.8.Kufanya usimamizi shirikishi katika vituo vya kutolea huduma na ngazi ya jamii,Kuwawezesha watoa huduma ngazi ya jamii kufanya tathimini ya hali ya lishe ,sambamba na kuwezesha utoaji wa mafunzo kwa watoa huduma ngazi ya jamii juu ya namna ya kutengeneza maziwa tiba kwa ajili ya matibabu ya utapiamlo’’.


Pamoja na mambo mengine,Bi Mkunda ameeleza mafanikio katika utoaji wa vidonge vya madini ya chuma na asidi ya Folik(FeFo) ambapo amesema kuwa vidonge vimetolewa katika vituo vyote vinavyotoa huduma za uzazi.


Naye mdau wa masuala ya lishe kutoka katika mradi wa USAID "Afya yangu – Mama na Mtoto"unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la Jh piego, Daktari Method Bulongeleje amesema kuwa suala la lishe ni suala muhimu katika kupunguza vifo vya watoto wa umri chini ya miaka 5.


Halmashauri ya Manispaa ya Temeke inasimamia utekelezaji wa mkataba wa lishe katika kata zote 23,kuimarisha hali ya lishe na kupunguza aina zote za utapiamlo ikiwemo udumavu,ukondefu,uzito pungufu na upungufu wa vitamin na madini ambapo imeweza kupunguza changamoto za kiafaya vikiwemo vifo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke