• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Sheria Ndogo ndogo

-TANGAZO LA SERIKALI  Na.   265   la tarehe  15/06/2018

SHERIA YA FEDHA ZA SERIKALI ZA MITAA

(SURA YA 290)

______

SHERIA NDOGO

______

 

(Zimetungwa chini ya kifungu cha 6(1)(u) na 16(1)

SHERIA NDOGO ZA (USHURU WA HUDUMA) ZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE ZA MWAKA 2018

Jina na mwanzo wa kuanza kutumika
 Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Ushuru wa Huduma) za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke  za mwaka 2018 na zitaanza kutumika baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali.
Matumizi
2. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la  Halmashauri ya Manispaa ya Temeke .
Tafsiri
Sura 212
Sura 290
3.   Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo:-
“Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni ya Afisa yeyote wa umma aliyeteuliwa na Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi.
 “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
 “Hesabu” maana yake ni jumla ya mauzo ya bidhaa, kazi au Huduma katika mwaka wa fedha.
“Kampuni” maana yake ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni Sura ya 212.
 
“Kipindi cha Hesabu” maana yake ni muda ambao mfanyabiashara anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara zake kwa Halmashauri.
 “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke au na Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi.
 “Mkusanya kodi” maana yake ni mtumishi au wakala aliyeteuliwa na Halmashauri kukusanya kodi.
 
 “Ushuru wa Huduma” maana yake ni Ushuru unaotozwa au kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni, taasisi ya biashara au mfanyabiashara kwa huduma anazopata kutokana na kutumia miundombinu ya umma inayomuwezesha kufanya biashara katika eneo la Halmashauri.
 
“Taasisi ya biashara” maana yake ni taasisi inayofanya biashara, kazi au kutoa huduma kwa lengo la kupata faida.
 
“Tawi la kampuni” maana yake ni tawi la kampuni lililosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni ambayo inafanya shughuli zake katika eneo la Halmashauri.
“Ukokotoaji” maana yake ni namna ya kuandaa kiasi cha Ushuru wa Huduma kinacholipwa kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha Sheria Ndogo hizi.
Utozaji wa Ushuru wa Huduma
4.  Halmashauri itatoza na kukusanya Ushuru wa Huduma kwa kampuni, tawi la kampuni, taasisi ya biashara, kwa kiwango kisichozidi asilimia sifuri nukta tatu (0.3%) kutokana na uzalishaji wa bidhaa, kazi na huduma zinazofanyika ndani ya eneo la Halmashauri ukiondoa Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na Kodi ya  bidhaa (excise duty).
Uwasilishaji wa taarifa kuhusu shughuli za kibiashara
5. -(1)  Mkurugenzi kwa taarifa ya kimaandishi, anaweza kumtaka mlipa kodi au mkusanya kodi yeyote kuwasilisha hesabu zenye taarifa kamili za shughuli za biashara zikionesha kiasi cha thamani ya kifedha ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, kutolewa, kuingizwa, kusambazwa, au kuuzwa kibiashara, taarifa ya fedha katika kipindi kisichozidi siku thelathini tangu tarehe ya taarifa hiyo.

(2)  Kila mfanyabiashara atawasilisha kwa Halmashauri taarifa sahihi za hesabu za mauzo ya kila mwezi husika na atalipa Ushuru wa Huduma kwa mujibu wa viwango vitakavyotokana na hesabu hizo na kwa wafanyabiashara wasio na vitabu vya hesabu watakokotolewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi.

(3)   Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu yeyote mwenye taarifa kuhusu mfanyabiashara anayepaswa kulipa Ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi, kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumika kama taarifa sahihi.
Uwezo wa kuingia kwenye jengo
6.-(1) Mkurugenzi anaweza kumwagiza kwa maandishi Afisa mwidhiniwa au Wakala  kuingia kwenye jengo au eneo la taasisi ya kibiashara au la mlipa au mkusanya kodi yeyote kwa nia ya kufanya uchunguzi na tathmini ya kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu na taarifa nyinginezo kama atakavyoona inafaa kufanyiwa uchunguzi kwa ajili ya kupata na kujua kiwango sahihi cha kodi anachotakiwa kulipa mlipa kodi au mkusanyaji kodi hiyo.

(2)   Kwa nia ya kupata taarifa kwa mujibu wa kifungu cha 6(1)  cha Sheria Ndogo hizi Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu yeyote kufika mbele yake au kwa Afisa Mwidhiniwa katika muda na mahali kadri atakavyoona inafaa.
Ukokotoaji wa Ushuru wa Huduma
7.  Halmashauri kwa kuzingatia taarifa zilizowasilishwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria Ndogo  hizi itakokotoa na kutoza Ushuru wa Huduma.
Uwasilishaji wa taarifa
8.-(1) Kila mlipa au mkusanyaji kodi ya huduma atatakiwa kutoa na kuwasilisha hesabu na kulipa kodi anayotakiwa katika muda anaopaswa kama ifuatavyo:-
Kwa waagizaji bidhaa kutoka nje ya nchi watalipa kodi katika muda kama itakavyokuwa imeelezwa na Kamishna wa Kodi ya Forodha na kodi ya mlaji;
Wazalishaji wa bidhaa za viwandani watalipa kodi kama itakavyokuwa imeelekezwa na Kamishna wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) isipokuwa haitakuwa zaidi ya muda wa kulipa Kodi ya mlaji au VAT.
Hesabu za mlipa kodi asiyewasilisha taarifa
9.  Iwapo mlipa kodi hajawasilisha majumuisho ya hesabu zake kwa mwaka wowote wa mapato aidha ametakiwa kufanya hivyo na Mkurugenzi anafikiri kwamba Mlipa kodi huyo ana wajibu wa kulipa kodi mwaka huo anaweza kwa kadri anavyo ona, kuamua kiwango cha hesabu za mlipa kodi huyo isipokuwa tathmini hiyo haitaathiri wajibu wowote wa mlipa kodi anayostahili kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi kwa kushindwa kwake uwasilishaji hesabu hizo.
Muda wa kulipa kodi
10. Kodi iliyotathminiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi italipwa ndani ya  kipindi cha siku thelathini tangu tarehe ya kufanya tathmini.
Uteuzi wa wakala
11.  Halmashauri inaweza kuteua Kamishna wa Kodi ya forodha au kodi ya mapato au wakala kutathmini na kukusanya kodi ya huduma na kuwasilisha kwa Halmashauri kwa wakati kama ilivyoelekezwa kwa lengo la kufanya tathmini, kukusanya na kupata kodi pamoja  na madeni yake.
Makosa
12. Mtu yeyote  atakuwa ametenda kosa iwapo;
atashindwa kuwasilisha hesabu sahihi;
atashindwa kuwasilisha nyaraka, maelezo au taarifa inayotakiwa kuwasilishwa kwa Halmashauri katika muda uliowekwa;
atashindwa kutunza kumbukumbu, kitabu au hesabu za mauzo yake;
atashindwa kuonyesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi.
akifanya hesabu za uongo kwa kupunguza au kutoa hesabu zisizokuwa sahihi
atatoa taarifa isiyokuwa sahihi kuhusu jambo lolote linaloweza kuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa kodi
ataandaa au kutengeneza au kusababisha kuandaliwa au kutengenezwa kwa vitabu vya uongo vya mahesabu au kumbukumbu;
atamzuia au atajaribu kumzuia Afisa Mwidhiniwa kutekeleza majukumu yake aliyopewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi.
Adhabu
13.   Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mbili (200,000/= na isiyozidi shilingi milioni moja (1,000,000/=) au kifungo kisichopungua  miezi kumi na mbili (12) na kisichozidi miezi ishirini na nne (24) au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo.
Kufifilisha kosa
14.    Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote faini isiyopungua shilingi laki mbili (200,000/=) na isiyozidi shilingi laki tano (500,000/=) iwapo mkosaji atakiri kosa kwa maandishi na kukubali kutekeleza wajibu wake pamoja na kulipa faini anayodaiwa.

JEDWALI

KUFIFILISHA KOSA

Limetungwa Chini ya kifungu cha 15

Mimi……………………………………..nakiri kwa hiari yangu mwenyewe mbele  ya……………………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwamba mnamo tarehe……………ya mwezi……………..mwaka ……………………….nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha ………………………cha Sheria Ndogo za (Ushuru wa Huduma) za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke za mwaka 2018.

Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri. niko tayari kulipa kiasi cha Ushuru wa Huduma ninachodaiwa pamoja na faini.

NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU

Leo tarehe…………………ya mwezi…………………Mwaka………………………..

Jina…………………………………..…..

Saini…………………………………….

Mbele ya:

Jina………………………………………..

Cheo………………………………………

Saini……...........................................……

 Nembo ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kilichofanyika tarehe 19 ya Mwezi 5 Mwaka 2017.                    

                

                                                                     Abdallah Jafari Chaurembo

                                                                    Mstahiki Meya wa Halmashauri ya

 Manispaa ya Temeke

                                                                        Nassib  Bakari  Mmbagga

                                                                      Mkurugenzi Halmashauri ya

Manispaa ya Temeke

 

   NAKUBALI:

Dodoma,                                                                      Mhe.Selemani Jaffo (Mb)

23th    Mei,   2018                                                   Waziri wa Nchi, Or Tamisemi                         

 

Matangazo

  • TANGAZO: KUFUNGA VITUO VYA DAYCARE January 29, 2023
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA January 06, 2023
  • TANGAZO: KUWASILISHA HESABU (TURNOVER) February 13, 2023
  • TANGAZO: KUWASILISHA HESABU (TURNOVER) February 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • KILIO CHA KIVUKO KATA YA MIANZINI CHAFIKA MWISH0

    March 25, 2023
  • "TUTAPAMBANA NA KIPINDUPINDU KWA USAFI" MHE. AMOS MAKALLA

    March 25, 2023
  • MTAKUWWA TEMEKE YADHAMIRIA KUDHIBITI VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO

    March 24, 2023
  • WANAHABARI WANA JUKUMU LA KUELIMISHA JAMII KUHUSU UGONJWA WA KIFUA KIKUU-MHE. UZAHILU

    March 24, 2023
  • Angalia zote

Video

RC MAKALLA AONGOZA ZOEZI LA USAFI MBAGALA
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke