Serikali imewahakikishia wafanyabiashara nchini mazingira mazuri ya kufanyia biashara huku akisisitiza kuondolewa kwa kodi na ushuru ambao ni kero kwa wafanyabiashara hao.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam leo alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa masoko katika manispaa ya Temeke.
Mh.Samia Suluhu alisema kuwa serikali katika kutekeleza kwa vitendo Ilani yake iliamua kuanzisha utaratibu wa vitambulisho vya wajasiriamali ambavyo vinawawezesha kulipa kwa awamu moja tu kwa mwaka na kusaidia kupunguza mzigo kwa wafanyabiashara hao.
"Lakini kama mlivyosikia Waziri Mkuu hivi punde alikuwa na mkutano na wawakilishi wa wajasiriamali wa Tanzania nzima ili kuangalia nini Serikali yenu inaweza kufanya kuboresha mazingira ya kufanya biashara".Aliongeza Mama Samia Suluhu Hassan.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais aliupongeza uongozi wa manispaa hiyo kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato lakini akiwakumbusha kuwa fedha hizo ziende kutatua kero na changamoto za wananchi.
Awali akimkaribisha Makamu wa Rais,Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh.Aboubakar Kunenge alieleza kuwa manispaa ya Temeke imepiga hatua kimaendeleo ukilinganisha na miaka iliyopita.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndg Lusubilo Mwakabibi kulia akitoa ufafanuzi wa jambo kwa makamu wa Rais Mama Samia wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo.
"Katika serikali hii ya awamu ya tano tunaona wilaya hii imepata maendeleo sana na inakuwa kwa spidi kubwa,kwa kweli nampongeza sana Mh.Rais."Alisema Mh.Kunenge
Katika ziara hiyo ambayo Mh.Makamu wa Rais alianzia katika wilaya ya Kigamboni,aliweza kukagua miradi ya barabara Kijichi, kituo cha kibiashara na soko Kijichi pamoja na masoko mengine ya ya Makangarawe, Mbagala kuu, pamoja na soko la Kilakala yote yakiwa katika manispaa ya Temeke.
Mhe Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwini Gondwe aliyenyosha kidole akitolea ufafanuzi jambo fulani mbele ya Makamu wa Rais.
Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.
Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam
Simu ya Mezani: +255 22-2928132
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz
Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke