• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Afya


 IDARA YA AFYA USTAWI WA JAMII NA LISHE 

KUANZIA JULY 2020 HADI APRIL 2021

 

  • UTANGULIZI
  • Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ni miongoni mwa Halmashauri 4 za Mkoa wa Dar Es Salaam. Halmashauri inaukubwa wa kilometa za mraba 240, na idadi ya watu inakadiriwa kuwa 1,958,973 (Wanaume 956,589 na Wanawake 1,002,384) na ongezeko la watu kwa mwaka ni 4.6% (NBS 2012).
  • Halmashauri ya Manispaa Temeke inajumla ya vituo 196 vya kutolea huduma za Afya, kati ya hivyo 25 vya Serikali, 4 vya Majeshi, 2 Mashirika ya Dini na 166 vya Watu Binafsi.
  • Jedwali 1: Vituo Vya kutolea huduma na umiliki wake
    • UMILIKI
    • Na 
    • Aina ya Vituo
    • Serikali
    • Majeshi
    • Watu Binafsi
    • Dini
    • Jumla 
    • 1
    • Hospitali
    • 2
    • 1
    • 4
    • -
    • 7
    • 2
    • Vituo vya Afya
    • 5
    • 1
    • 12
    • -
    • 18
    • 3
    • Zahanati
    • 18
    • 1
    • 88
    • 2
    • 109
    • 4
    • Kliniki
    • -
    • -
    • 37
    • -
    • 37
    • 5
    • Maabara
    • -
    • -
    • 25
    • -
    • 25

    • Jumla 
    • 25
    • 3
    • 166
    • 2
    • 196

    • IDADI YA WATUMISHI WA IDARA AFYA
    • Manispaa ya Temeke ina jumla ya Watumishi 752 (63%) wa Idara ya Afya, ambapo mahitaji halisi ni Watumishi 1,196 na hivyo kupelekea kuwa na upungufu wa Watumishi 444 (37%)
    • Ili Vituo viweze kuendelea kutoa huduma kama kawaida tumeajiri Watumishi 50 wa Mkataba kwa Vituo vyenye uhitaji mkubwa.
    • Idara ya afya inaendelea na zoezi la upandishwaji vyeo kwa watumishi baada ya kupata barua yenye kibali cha mwaka 2018/19, 2019/20 na 2020/21. Jumla ya watumishi 321 wameshaandikiwa barua na zoezi la upandishaji linaendelea kwakufwata utaratibu unaotakiwa.  Sambamba nazoezi la kubadilishwa vyeo kwa misingi ya elimu nalo linaendelea kibali cha ikama kinachotumia pia ni cha mwaka 2018/19, 2019/20 na 2020/21.
    • Vituo vyote 24 vyakutolea huduma ya afya vimefungwa mfumo wa GoTHOMIS kwaajili yakukusanyia taarifa za  wateja wanaohudumiwa kituoni.
    • Halmashauri ina magari ya kubebea wagonjwa manne ambayo yapo kwenye hali nzuri. Mpango mkakati wa idara nikuweka kwenye bajeti ya kila mwaka bajeti yakununua gari lakubebea wagonjwa ili tuwe na magari yakutosha na tuweze kuepukana na changamoto yakukosa magari pindi inapotokea dharura ya aina yoyote.

  • Hali ya utolewaji wa huduma
  • Huduma ya Afya ya uzazi na Mtoto
  • Katika Mwaka 2020 jumla ya kina mama waliojifungua walikuwa 35,474, waliojifungua kwa njia ya upasuaji walikuwa 3,920 na njia ya kawaida walikuwa 31,554.

    Manispaa ina jumla ya vituo 95 vinavyotoa huduma ya Afya ya uzazi na mtoto, kati ya hivyo vituo 90 vinatoa huduma ya wajawazito, vituo 37 vinazalisha na vituo 93 vinatoa huduma za uzazi wa mpango.


    • Huduma za Wazee
    • Halmashauri ya Manispaa ya Temeke inaendelea kutoa huduma bora kwa Wazee kwa kutoa matibabu bure kwa wazee wasio na Bima na imeweza kuwatambua Wazee kutoka Kata 23 za Manispaa ya Temeke ambapo kwa mwaka 2018 jumla ya Wazee 15,201 walitambuliwa (Me 8,622 na Ke 6,579) kati ya hao Wazee 13,158 (87%) walipatiwa vitambulisho (Me 6,829 na ke 6,329). Zoezi la utambuzi na kuwatengenezea vitambulisho ni endelevu.
    •  
    • Huduma za VVU 
    • Idara ya Afya Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kusimamia huduma za kuzuia maambukizi ya VVU na UKIMWI  kwa kupitia  huduma za kuzuia maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (PMTCT), huduma za upimaji wa VVU/UKIMWI kwa hiyari (HTC), huduma za upimaji wa VVU/UKIMWI kwa ushawishi (PITC) na Matibabu na ufuatiliaji wa watu waliogundulika kuwa wana maambukizi ya VVU (CTC).
    •  
    • Idadi ya Vituo vya kulotelea huduma ya tiba na matunzo vipo 60, Vya Serikali 24  na  Binafsi 36. PMTCT stand alone 1, CTC alone 1, (Both CTC na PMCTC jumla 58)
    • Idadi ya Watu wanaoishi na VVU mpaka kufikia mwezi April 2021  ni 47,724 ikiwa 13,591 ni Wanaume na 34,133 ni Wanawake.
    • Huduma zitolewazo kwa wagonjwa/wateja wa VVU/UKIMWI ni pamoja na huduma za tiba, Uuguzi, Kijamii na Kisaikolojia, Lishe na Kinga.
    • Upatikanaji wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi hadi April 2021
    • Hali ya upatikanaji wa dawa muhimu (essential medicines) na vifaa tiba  hadi kufikia  April 2021 ni asilimia 95.4.kutoka  60% kwa mwaka 2015.
    •  
    •  
    • Jedwali 2: Kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa
      • CHANZO CHA FEDHA
      • 2015/16
      • 2020/21
      • Uchangiaji,NHIF, Ichf
      • 732,458,594/=
      • 2,213,082,757/=
      • Basket
      • 585,557,676/=
      • 705,118,893/=
      • MSD
      • 787,151,557/=
      • 1,411,790,522/=

      • Pia, serikali imetoa tayari fedha za mfuko wa pamoja (basket fund) kwa vituo vya kutolea huduma za afya katika halmashauri kwa robo ya kwanza na pili ambapo asilimia 35 imenunua Vifaa tiba, Dawa na Vitendanishi.
      • Kwa upande wa Maabara huduma ya ukusanyaji wa damu kupitia MKOBA tulifanikiwa kukusanya chupa za damu 2,519 sawa sawa na 89.9% ya lengo la ukusanyaji chupa za damu 2,800 mwaka 2020.
      • Matarajio ni kuongeza bajeti katika eneo hili la ukusanyaji ili malengo ya ukusanyaji damu yafanikiwe kwa 100%.
      • Utekelezaji wa uanzishwaji wa maduka ya dawa Hospitali za Halmashauri.
      •  
      • Katika Manispaa yetu, uanzishwaji duka la dawa katika Hospitali ya Halmashauri ulikwama kutokana na ufinyu wa nafasi. Ila Hospitali iliweza kuboresha dirisha la dawa la wateja wa Bima za Afya kwa kulifanyia ukarabati na kuwekeza mtaji wa  Tshs. 67,350,000.
      • Mpango uliopo mwaka huu ni kuanzisha duka hilo katika kituo cha Afya cha Yombo Vituka, na mwakani katika vituo vya afya vya Maji Matitu na Buza. Pia, manispaa ipo katika mpango wa kujenga hospitali kubwa ya halmashauri itakayokuwa na miundombinu yote ikiwa ni pamoja na duka la dawa la jamii.
    •  


      • Utendaji kazi wa mfumo wa MSHITIRI katika utoaji huduma.
      • Pamoja na serikali kutoa fedha za ruzuku MSD, bado kumekuwepo na ukosefu wa bidhaa muhimu za afya na hivyo vituo kulazimika kujazia kupitia mfumo mshitiri.
      • Ingawa Mshitiri amekuwa akijitahidi kuziba pengo hilo, bado na yeye anakabiliwa na mapungufu mbalimbali kama vile;- ukosefu wa vitendanishi vya maabara kama vile controls na kutoleta bidhaa za Afya katika ukamilifu, kwani amekuwa akileta katika mafungu, n.k
      • Hivyo basi, ukiachilia mafanikio ya mfumo mshitiri, anapaswa kuboresha zaidi kwani utendaji wake katika utoaji wa huduma za dawa katika manispaa yetu ni asilimia 76
    •  

       


      • Utekelezaji wa Mfuko wa Ichf
      • Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa katika Manispaa ya Temeke ulianza rasmi Januari 2019 na mpaka sasa Mfuko una Wanachama 18,342 (4.1%), na michango ya Wanachama mmoja mmoja ni Tshs. 102,480,000/= na michango kwa Kaya ni Tshs. 502,360,000/= hivyo kufanya  jumla ya michango yote kuwa Tshs. 604,840,000/=
      • Jumla ya pesa zilizopelekwa vituoni mpaka sasa ni Tshs. 60,752,153.57/=
      •  
      •  
      • 6. TAARIFA YA KITENGO CHA CHANJO
      • Kitengo cha chanjo kinashughulikia Usimamizi wa Hudumaza Chanjo na Pia kufuatilia Magonjwa yanayozuilika kwa Chanjo.
      • Katika Manispaa ya Temeke  kwa mwaka  huu kuna  jumla ya vituo 96 vinavyotoa huduma za Chanjo (25 kati ya hivyo vinamilikiwa na  Seriklai na Vituo 71 vinamilikiwa na watu binafsi pamoja na mashirika ya dini .
      • Chanjo za watoto hutolewa  vituoni siku zote za kazi kuanzia  jumatatu hadi ijumaa .
      • Walengwa wa Chanjo kwa huu ni  Watoto chini ya Mwaka mmoja ni 45,173,Wajawazito ni 50,061,Watoto waliozaliwa hai 50,061,wasichana wenye umri wa Miaka 14 ni 13,451.
    • Katika kipindi cha Mwezi Jan,Februari na Machi  2021 kiwango cha uchanji chanjo ya bOPV na MR,kilikuwa chini 76% kutokana na ukosefu mkubwa wa Chanjo hizo nchini.

      Kiwango cha uchanjaji kilifikia 102%,na wasichana waliochanjwa HPV1 walikuwa 4,981 (111%) ,,MR 1 watoto 19,430 (129%)

      iii.Hali ya Uchanjaji/kiwango cha chanjo.

      Hadi leo hii  chanzo zote za Watoto pamoja na Td za wajawazito za zipo  za kutosheleza muda wa miezi 2 isipokuwa Chanjo za PCV ambazo zipo za kutumia muda wa wiki 3 tu.

      Katika miezi miwili  ya nyuma (Jan,Febr, na March  kulikuwa  na upngufu mkubwa wa chanjo za kuzuia Magonjwa ya Watoto kama MR,PCV,PENTA na TT.na ukosefu wa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (bOPV)

      ii.Hali ya Upatikanaji wa Chanjo katika Halmashauri.


  • 7.TAARIFA YA MIRADI YA MAENDELEO
  • Jedwali Na. 4. Taarifa ya miradi ya maendeleo iliyopo hadi kipidi hiki.

NO.

JINA LA KITUO

AINA YA KITUO

UMILIKI

AINA YA MRADI

MWAKA WA KUKAMILISHA MRADI

CHANZO CHA FEDHA

GHARAMA ZA MRADI

MANUFAA YA MRADI


YOMBO VITUKA
KITUO CHA AFYA
SERIKALI
Ujenzi wa jengo la Ghorofa mbili

2019

Mapato ya ndani (own source)

2,125,530,460.00

Kumamilika kwa jengo hili kutapunguza mlundikano wa wagonjwa kwenye majengo ya zamani. Huduma zitakazoboreshwa ni pamoja na huduma za   upasuaji,maabara,kulaza, wodi ya watoto wachanga na wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU).

2.

BUZA
KITUO CHA AFYA
SERIKALI
Ujenzi wa jengo la Ghorofa mbili

2020

Benki ya Dunia kupitia mradi wa DMDP

2,153,509,631.31

Kumamilika kwa jengo hili kumepunguza mlundikano wa wagonjwa kwenye majengo ya zamani. Pia huduma mpya za upasuaji, afya ya kinywa na meno,kulaza, wodi ya watoto wachanga na wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU) zitaanzishwa.

Ununuzi wa Gari la Wagonjwa (Ambulance)

2020

Benki ya Dunia kupitia mradi wa DMDP

216,952,347.37

Huduma za rufaa zimeimarishwa katika manispaa ya Temeke wagonjwa wagonjwa wanapata huduma ya rufaa kwa wakati.

3.

MAJI MATITU
KITUO CHA AFYA
SERIKALI
Ujenzi wa Jengo la Maabara

2019

Fedha  kutoka Benki ya Dunia kupita TAMISEMI

87,423,769.96

Huduma za vipimo vikubwa vya maabara zimesogezwa karibu na wananchi.

Ujenzi wa chumba cha upasuaji

2019

Fedha  kutoka Benki ya Dunia kupitia TAMISEMI

136,975,055.00

Huduma za upasuaji kwa akina mama zimeongezeka kutoka 0 (2018) hadi kufikia 230 mwaka (2020). Januari-Machi 2021upasuaji (CS) 110.
Ujenzi wa wodi ya wazazi

2019

Fedha  kutoka Benki ya Dunia kupitia TAMISEMI

156,403,694.74

Kukamilika kwa majengo haya kumesaidia kuongezeka kwa huduma ya kujifungua kituoni kutoka 314 mwaka 2015 hadi kufikia 2874 (2020).Januari-Machi 2021 huduma ya kujifungua ni 684
Uchimbaji wa kisima

2019

NURU Foundation

15,149,256.40

Kituo kinapata maji safi na salama.

4.

CHARAMBE
ZAHANATI
SERIKALI
Ujenzi wa zahanati ya charambe

2020


730,536,235

Kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati hii imepunguza mlundikano wa Wagonjwa katika hospitali ya Mbagala Rangitatu.

5.

MBANDE
ZAHANATI
SERIKALI
Ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi

2021

Ruzuku kutoka serikali kuu

50,000,000.00

Wazazi watapata huduma bora, kwa usiri na utulivu wa huduma utaongezeka  katika vyumba vya kujifungulia

6.

MIBURANI
ZAHANATI
SERIKALI
Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje

2020

Mapato ya ndani (own source)

100,000,000.00

Kukamilika kwa jengo hili itasaidia kupatikana huduma za afya karibu na wananchi,kata hii haikuwa na kituo cha kutolea huduma za afya cha serikali.

Ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi

2021

Ruzuku kutoka serikali kuu

50,000,000.00

7.

TANDIKA
ZAHANATI
SERIKALI
Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje

2020

Mapato ya ndani (own source)

100,000,000.00

Kukamilika kwa jengo hili itasaidia kupatikana huduma za afya karibu na wananchi,kata hii haikuwa na kituo cha kutolea huduma za afya cha serikali.


Ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi

2021

Ruzuku kutoka serikali kuu

50,000,000/=

8.

MBAGALA KIZUIANI
ZAHANATI
SERIKALI
Ujenzi wa jengo la mama na mtoto

2021

Fedha za uchangiaji

72,130,000.00

Kukamilika kwa jengo hili huduma za mama na mtoto zitaimarika kituoni

9.

HOSPITALI YA WILAYA TEMEKE
HOSPITALI YA WILAYA
SERIKALI
Ujenzi wa Hospitali
2021 - 2022
Mapato ya ndani

1,500,000,000.00

Hospitali itapunguza msungamano katika Hospitali ya Mbagala Rangi tatu na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke,. Pia wananchi watapata huduma muhimu za afya kwa urahisi karibu na makazi yao.



  • 8      MAFANIKIO                        
  • Ongezeko la hudhurio la nne  kutoka  43.3% mwaka 2015 kufikia 98.7% Mwaka 2020
  • Ongezeko la wateja kliniki 69% mwaka 2018 Kufikia 92% mwaka 2020.
  • Ongezeko la wateja wajawazito waliopewa dawa za kuzuia Malaria IPT2  67.8% 2015 kufikia 146% 2020
  • Ongezeko la wateja wajawazito waliopewa dawa za kuongeza damu. (FEFO) 60% 2015 kufikia  92% 2020
  • Ongezeko la kiwango cha wajawazito waliopimwa VVU 97% 2016 kufikia 100% mwaka 2020
  • Ongezeko la vituo vya CemONc toka 3 mwaka  2015 kufikia 5 mwaka 2020
  • Ongezeko la vituo vinavyotoa huduma rafiki ya vijana toka vituo 3-  mwaka 2015 kufikia vituo 31  mwaka 2020
  • Kupunguza vifo vya watoto  mwaka  mmoja (mortality rate} mwaka 2015   5/1000 kufikia  2.6/1000 mwaka 2020
  • Kupunguza vifo vya watoto wachanga siku 0-28 kutoka 12/1000 mwaka 2018 kufikia 6/1000 mwaka  2020
  • Jumla ya Mabaraza 166 ya wazee yameanzishwa ngazi ya Wilaya lipo moja, ngazi ya Kata yapo 23, ngazi ya Mitaa yapo 142.

Wateja wote waliogundulika na maambukizi ya VVU wameweza kuanzishiwa dawa kwa 99.3%

Katika Wateja wanaotumia dawa za ARV 94.7% virusi vyao vimefubazwa hivyo uwezakano wa kuambukiza wengine ni wa kiwango kidogo

Waandikishaji wa iCHF wapo katika Kata zote za Manispaa ya Temeke na Vituo vya kutolea huduma za Afya vya Serikali.

Huduma za iCHF zimeanza kutolewa katika baadhi ya Hospitali binafsi ili kurahisisha  upatikanaji wa huduma mfano Hospitali ya Hafford Temeke.


  • 9      CHANGAMOTO
  • Wajawazito  kuchelewa kuanza kliniki zaidi ya wiki 12 (Late booking) 23%
  • Ongezeko la vifo vitokanavyo na uzazi kutoka 57/100,000 2019 kufikia 62/100,000 mwaka 2020
  • Kiwango cha chini cha wateja wanaotumia njia za kisasa za uzazi wa mpango 19%
  • Upatikanaji hafifu wa dawa za kuongeza damu (FEFO) katika vituo vyetu

Fedha toka Sekta Kuu kuchelewa kutolewa hivyo kuathiri utoaji wa huduma

Bajeti ndogo ya Idara ikilinganishwa na mahitaji halisi

  • Upungufu mkubwa watoa huduma za Afya 37%
  • Idadi ndogo ya uandikishaji wa Wanachama wapya  (4%) tu.
  • Uelewa mdogo wa Wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii


  • 10.      MIKAKATI YA KUONDOA CHANGAMOTO HIZO
  • Kuendelea kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuhudhuria kliniki mapema kupitia kamati za Afya za Vituo.
  • Kuendelea kukusanya fedha za uchangiaji na kudhibiti mianya ya upoteaji fedha kwa kuunganisha vituo vyote na mifumo ya GePG.
  •  
  • iCHF kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyote vya Halmashauri kuanzia ngazi ya Mitaa, Kata, Manispaa na Baraza la Madiwani.
  • Kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kujiunga na iCHF hususani kwenye mikusanyiko kama masokoni, Vituo vya mabasi, vituo vya kutolea huduma za Afya  na Mashuleni. Pia kutoa elimu kwa njia za Radio, Televisheni n.k.
  • Kuwatambua na kuendelea kuwatumia wadau ili waweze kuchangia  mfuko kwa kuwatolea fedha familia zisizojiweza.



                                                                                                                Dr Gwamaka S. Mwabulambo

MGANGA MKUU WA MANISPAA

TEMEKE 

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TANGAZO

    April 08, 2025
  • TUTAENDELEA KUKUKUMBUKA HAYATI SHEIKH ABEID AMANI KARUME

    April 07, 2025
  • KAMPENI YA SOMA NA MITI YATEKELEZWA

    April 04, 2025
  • TEMEKE YAJIDHATITI KUTEKELEZA MIRADI YA MIKUBWA YA MAENDELEO

    April 03, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke