Katika kuhakikisha manispaa ya Temeke inaendelea kuwa safi kimazingira,watendaji wa serikali za Mitaa wameagizwa kusimamia zoezi la usafi kikamilifu.
Akizungumza na Watendaji hao wakati wa kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa,Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ndugu Lusubilo Mwakabibi amesema kuwa mtendaji yeyote ambaye hatasimamia zoezi hilo ajihesabie kuwa hana nafasi katika Manispaa hiyo .
"Mimi sijaja kupendwa hapa,ninachokifanya hapa ni kusaidia kuwaondoa watu kutoka katika umaskini na kuwafanya kuwa na hali bora ya maisha,uchafu ni umaskini".Alisema Mwakabibi.
Mwakabibi amewataka Watendaji hao kujiwekee utaratibu mzuri wa kusimamia usafi katika maeneo yao na kwamba sheria zipo zinazowaongoza kwa wale wanaokaidi kufanya usafi.
"Inashangaza sana unapopita mtaani na kukuta takataka zimezagaa na mitaro kuziba na wewe mtendaji upo,nipo 'serious' nitakuondoa".Alisisitiza Mkurugenzi Mwakabibi.
Mkutano huo uliandaliwa na Mkurugenzi wa Manispaa kwa ajili ya kuwakumbusha watendaji kuhusu masuala mbalimbali katika utendaji wao ikiwemo suala la usafi wa mazingira katika maeneo yao.
![]() |
ReplyForward |
Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.
Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam
Simu ya Mezani: +255 22-2928132
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz
Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke