Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ina Idara mbili zinazosimamia masuala ya elimu na kiwango cha elimu kinachotolewa katika mipaka yake.
ambazo ni:
1. Elimu Msingi na
2. Elimu Sekondari
1. Huduma zinotolewa na Idara ya Elimu
Zipo huduma mbalimbali zinazotolewa na Idara ya Elimu Msingi na Elimu Sekondari katika halmashauri ya manispaa ya Temeke nazo ni;-
. Kuboresha kiwango cha Elimu.
. Kuhakikisha michezo mashuleni na kuwepo kwa vifaa vya michezo mashuleni.
. kusimamia utekelezaji wa sera ya elimu Msingi bure.
. Ukusanyaji wa takwimu mbalimbali zinazohusika na elimu.
. Kusimamia zoezi la uhamisho wa wanafunzi kutoka Wilaya moja kwenda Wilaya nyingine na ndani ya Manispaa ya Temeke.
. Kushughulikia mahitaji na maslahi ya walimu ndani ya Manispaa ya Temeke. Mfano;- Likizo, madaraja nakadharika.
. Kutembelea na kukaguua miundombinu ya mashule na kutoa ushauri kwa Mkurugenzi pale panapohitajika msaada wake wa utekelezaji.
. Kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika utoaji wa huduma mbalimbali mashuleni. Mfano;- Watoto wenye mazingira magumu Mshuleni.
Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.
Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam
Simu ya Mezani: +255 22-2928132
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz
Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke