Ofisi ya habari na uhusiano ya halmashauri ya manispaa ya Temeke inapenda kuwatangazia wakazi wa Temeke na umma kwa ujumla kuwa kuanzia tarehe 12/09/2019 hadi tarehe 31/10/2019 tutafanya ziara kutembelea kata za manispaa ya Temeke, katika ziara hizo tutawahoji waheshimiwa madiwani,watendaji wa kata na wananchi kuhusu miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na serikali katika kata zao, tutawasikiliza wananchi pamoja na kupokea maoni yao .
Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.
Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam
Simu ya Mezani: +255 22-2928132
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz
Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke