Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke Bwana Lusubilo Mwakabibi amesema kuwa hatasita kuvitaifisha viwanja na maeneo yasiyoendelezwa.
Mkurugenzi huyo aliyasema hayo ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi kuhusu umiliki na uendelezaji wa maeneo katika Manispaa hiyo.
"Kama una eneo lako eneo la Mbagala,Kijichi au Chamazi na hujaviendeleza,hivi viwanja tunaenda kuvifuta na usihangaike kuzunguka huko na huko,mimi ndiye mwenyekiti wa ardhi katika manispaa ya Temeke"Alisisitiza Bw.Mwakabibi
Huku akinukuu vifungu vya sheria ya Ardhi ya mwaka 1982,Bw Lusubilo Mwakabibi alisema kuwa hawatamuonea mtu na wanafanya kwa mujibu wa sheria.
Halmashauri ya Manispaa hiyo imekuwa ikipoteza mapato yatokanayo na kodi za Ardhi,majengo pamoja na vibali vya ujenzi.
Aidha Bw.Mwakabibi aliwatahadharisha matapeli ambao hutengeneza nyaraka bandia kwenye viwanja visivyoendelezwa na kujifanya wamiliki halali wa viwanja hivyo.
"Kuna watu wamezungusha uzio zaidi ya miaka 20 hatutakubali mambo haya,na hii husababisha migogoro ya ardhi".Alisema Mkurugenzi huyo.
Tayari mpaka sasa mchakato wa kuvifutia hati za umiliki viwanja 62 katika maeneo ya Mtoni Kijichi,Mbagala na Chamazi umeanza.
Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.
Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam
Simu ya Mezani: +255 22-2928132
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz
Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke