• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

KAMATI YA LISHE WILAYA YAKETI KIKAO CHA ROBO YA KWANZA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

Posted on: November 25th, 2025

Na: Joanita Joseph, TMC Habari


Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Temeke leo Novemba 25, 2025 imeketi Kikao cha kawaida ambacho ni mahsusi kwa ajili ya kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Robo ya kwanza (Julai-Septemba) Mwaka wa fedha 2025/2026.


Wajumbe wa kamati hiyo wamewasilisha Taarifa zao za utekelezaji kupitia Idara na Vitengo vyao ikiwemo mafanikio yaliyofikiwa pamoja na changamoto mbalimbali ili ziweze kujadiliwa na kutafuta namna sahihi ya kutatuliwa na hatimaye kufikia malengo.


Akizungumza katika Kikao hicho Ndg. Yahya Madenge Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Temeke na Mwenyekiti wa Kikao hicho mara baada ya kupokea taarifa amesisitiza Watoto kuendelea kupatiwa Chakula Mashuleni ili kujiepusha na madhara yatokanayo na ukosefu wa lishe lakini kuongeza ufanisi wa kujifunza wanapokuwa katika Masomo yao hatimaye kukuza Ufaulu.


"Chakula mashuleni si tu ni lishe pekee, bali ni hamasa kwa mtoto hata kuhudhuria shuleni na kujifunza, tuendelee kuhamasisha wazazi kuchangia chakula mashuleni ili watoto wale"  alisema Ndg. Madenge.


Kwa upande wake Bi. Happy Nkunda, Afisa lishe Manispaa ya Temeke amesema Idara ya Afya imekuwa ikisimamia kikamilifu Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ikiwemo kuwapatia wajawazito vidonge vya madini ya chuma na Asidi ya foliki (feFo) ili kuzuia mtoto kuzaliwa na ulemavu, kuendelea na upimaji wa hali ya lishe, matibabu na elimu ya lishe katika Vituo vya kutolea huduma za Afya, pamoja na kuendelea kuhamasishana juu ya suala la ulaji Mashuleni.


Hata hivyo Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa malengo kupitia Idara na vitengo husika na kuwekeana mikakati bora zaidi ya utendaji katika kuhakikisha hali ya lishe inazidi kuimarika wilayani Temeke.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAWAKILISHI KUTOKA WORLD BANK NA TIMU YA UTEKELEZAJI YA MRADI WA DMDP II WAFANYA MKUTANO WA PAMOJA

    November 25, 2025
  • KAMATI YA LISHE WILAYA YAKETI KIKAO CHA ROBO YA KWANZA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    November 25, 2025
  • CRDB BANK YAKABIDHI MADAWATI SET 30 SHULE YA SEKONDARI DOVYA

    November 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI KWA KUTEULIWA NA KUTHIBITISHWA KUWA WAZIRI MKUU MH. MWIGULU NCHEMBA

    November 14, 2025
  • Angalia zote

Video

TEMEKE YAWEZEKEZA BILIONI 35 SEKTA YA ELIMU PEKEE MWAKA WA FEDHA 2025/26
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke