Kufuatia muongozo mpya wa Serikali kuhusu ukusanyaji wa kodi za majengo,ushuru wa mabango na vitambulisho vya wajasiriamali kusimamiwa na Wakurugenzi wa halmashauri;uongozi wa manispaa ya Temeke umeanza kujiandaa kutekeleza agizo hilo.
Akiongea na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa manispaa hiyo Bw.Lusubilo Mwakabibi alisema kuwa wameandaa utaratibu utakaowawezesha kutambua idadi kamili ya nyumba zilizopo kwenye Manispaa hiyo ili kuweza kufanikisha zoezi la ukusanyaji wa kodi hiyo ya majengo.
"Leo hii tarehe 3 mwezi huu wa pili nimeita watendaji wangu wote wa mtaa na kata tupange namna ya kwenda kukusanya mapato".Alisema Bw.Mwakabibi
Aidha Bw.Lusubilo alitoa maelekezo kwa watendaji wa mitaa na kata kuhakikisha zoezi hilo la utambuzi wa majengo linafanyika kwa wakati ili kurahisisha zoezi hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa watendaji wa kata wa wilaya ya Temeke Bw.Anzamen Mandari alisema baada ya kupata maagizo hayo ya Mkurugenzi,watahakikisha hakuna nyumba au jengo litakaloachwa bila kulipa kodi.
Naye Afisa mtendaji wa kata ya Buza Bi Hulda Ulomi alimpongeza Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweka msisitizo katika suala zima la ulipaji wa kodi ambazo ndizo zinasaidia kufanya miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
"Tumekuja hapa kupata maelekezo na tutahakikisha kuwa haya tuliyoelekezwa leo tunayafanyia kazi".Alibainisha Bi Mtendaji huyo.
Februari mosi mwaka 2021 Serikali kupitia Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikalu za Mitaa Mh.Suleimani Jafo alitoa muongozo mpya wa serikali juu ya ukusanyaji wa kodi mbalimbali kurudishwa chini ya wakurugenzi wa Halmashauri Nchini.
Baadhi ya watendaji wa Kata na Mitaa wakiwa katika kikao kazi ukumbi wa Manispaa Iddy Nyundo mapema leo
Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.
Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam
Simu ya Mezani: +255 22-2928132
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz
Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke