Viongozi wa vyama na Serikali wametakiwa kuacha malumbano na badala yake wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Temeke Bi Almish Hassal alipokuwa kwenye ziara na kamati ya siasa ya Wilaya hiyo kukagua miradi ya maendeleo.
"Nakupongeza sana Mh.Diwani wa kata hii ya Kilungule Mh.Saidi Fella kwa jinsi unavyokaa na kamati yako ya maendeleo ya wilaya na kusikiliza kero za wananchi kwa pamoja".Alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh.Godwin Gondwe aliwahakikishia wananchi wa Wilaya hiyo kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kutatua changamoto za wananchi na ikiwezekana kuzimaliza kabisa.
"Kwa mfano mdogo tu tokea Uhuru wilaya hii ilikuwa na barabara ya lami kilometa 70 tu lakini kwa kipindi cha miaka mitano tu yw Mh.Magufuli ametengeneza zaidi ya kilometa 90".Alibainisha Mh.Gondwe.
Akimkaribisha Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Temeke,Diwani wa kata ya Kilungule Mh.Saidi Fella aliiomba serikali kujenga shule ya msingi pamoja na zahanati ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya na elimu.
Kamati hiyo ya siasa imeweza kutembelea miradi mbalimbali katika wilaya hiyo ikiwemo kituo cha afya Buza,soko la Makangarawe pamoja na eneo la Muhimbili Chamazi ambapo panatarajiwa kujengwa hospitali ya Wilaya.
Matukio katika picha wakati wa ziara ya kamati ya Siasa (W) Temeke.
Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.
Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam
Simu ya Mezani: +255 22-2928132
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz
Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke