• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

DC MATINYI AZINDUA RASMI ZOEZI LA ARDHI CLINIC (HATI PAPOHAPO)

Posted on: September 20th, 2023

Na: Joanita Joseph -TMC Habari


Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa

Mobhare Matinyi ametoa wito kwa wakazi wa Temeke kujitokeza kwa wingi kwa ajili kuboresha usalama wa milki za ardhi zao ikiwemo kugawiwa hati papo hapo.


Mhe. Matinyi ameyasema hayo leo Septemba 20, 2023 kwenye mkutano wa uzinduzi wa Ardhi Clinic, zoezi ambalo lipo chini ya Mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi (LTIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi.


Mhe. Matinyi amemshukuru Mhe. Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kutafuta fedha kwa ajili ya kuboresha milki za ardhi nchini na kuwataka Wananchi kutumia fursa hiyo muhimu.


"Mheshimiwa Rais ametafuta fedha kwa ajili ya kuboresha milki za ardhi kwenye maeneo yetu, hivyo Wananchi tutambue umuhimu na tujitokeze kwa wingi, jambo zuri huduma zote zinatolewa kielektronikia unapewa hati yako na rekodi zako zinahifadhiwa kidigitali " alisema DC Matinyi


Kwa upande wake mwakilishi wa mradi Bi. Aisha Masanja amesema kuwa zoezi hilo litadumu kwa siku 25 na litapita kwenye mitaa mitano.

"Tumeanzia hapa Mbagala kuu mashariki, na tutakuwa hapa viwanja vya Zakhiem kuwahudumia wananchi kwa muda wa siku tano, na baada ya hapo zoezi hili litahamia kwenye mitaa mingine ambayo ni Buza, kisewe, Mwembebamia,na Mianzini" alisema Bi. Aisha


Mara baada ya Mkuu wa wilaya kuzindua rasmi zoezi hilo, alikabidhi kwa Wananchi hati miliki zilizoshughulikiwa papo hapo.


Mradi wa uboreshaji usalama wa Milki za ardhi (LTIP) unalenga kutatua changamoto zote zinazokabili urasimishaji ardhi nchini ikiwemo kupanga na kupima maeneo yanayoyohitaji leseni za makazi na hati Miliki, kurahisisha gharama za upimaji, kutoa hati na leseni za makazi pamoja na kuboresha miundo mbinu ya ardhi kwa nchi nzima.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke