• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

KAMANDA NG'AZI AANZA NA STENDI YA KIJICHI TEMEKE

Posted on: November 8th, 2022

Na; Nassoro Rashid

TMC Habari

Leo Novemba 8, 2022 kamanda mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania Ramadhani Ng'anzi amefanya ziara katika stendi ya mabasi yaendayo kusini na mikoa ya jirani nje ya Dar es salaam iliyopo Kijichi wilaya ya Temeke kuona maendeleo ya stendi hiyo.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo kamanda Ng'azi amesema baada ya kukabidhiwa ofisi hapo jana ameona leo atoke nje ya ofisi kwa kufanya ziara Temeke hususani katika stendi hiyo na kufanikiwa kuona mradi huo umekamilika kwa kiasi kikubwa huku kukiwepo matengenezo kwa baadhi ya changamoto ndogo ndogo zilizopo.

"Changamoto zilizopo zinafanyiwa ufumbuzi kwani mradi utakapokamilika utakidhi matakwa ya usafirishaji bora, hivyo kwa sasa hatuna cha kupoteza kwani Jeshi la polisi lipo tayari kuona mradi huu unafanikiwa, na tutahakikisha magari yote yanafika Kijichi". Alisema kamanda Ng'azi

Kadhalika kamanda Ng'azi ametoa rai kwa mawakala wa mabasi waliopo Stendi ya Kijichi kufanya kazi zao kwa uadilifu, uaminifu pamoja na nidhamu na haki kwa kila mmoja na hawatakuwa tayari kuona yoyote anavunja sheria na utaratibu wa usalama barabarani.

"Lengo letu hasa kufanya barabara zetu zipitike kwa usalama kuanzia Januari mosi mpaka Disemba 31 bila ya matukio yoyote ya ajali kwa wasafiri wote, pia ziwawezeshe wananchi kunufaika na kufaidika kwa kusafirisha mazao yao na bidhaa zingine". Alisema Kamanda Ng'azi

Sambamba na hayo pia kamanda Ng'azi amesema yupo tayari kushirikiana na Mkuu wa Wilaya wa Temeke Mhe. Jokate pamoja na Mkurugenzi Mabelya kwani wote wana majukumu makubwa ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo kamanda Ng'azi amechukua majukumu hayo mara baada ya mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kufanya mabadiliko madogo ya kumuhamisha kutoka kamanda mkuu wa mkoa wa Mwanza na kuwa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke