• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Kamati ya siasa Yafurahishwa na Utekelezaji wa ilani Temeke.

Posted on: May 30th, 2019

Kamati  ya siasa  mkoa wa Dar es Salaam ikisikiliza maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa  manispaa ya Temeke  kuhusu ujenzi  wa Jengo la ghrorofa mbili linalojengwa katika zahanati ya Yombo vituka.Jengo hili  linajengwa kwa mapato ya ndani, litakapokamilika zahanati hiyo inatarajiwa kupandishwa hadhi na kuwa kituo cha afya

Kamati ya Siasa Mkoa wa Dar es Salaam ikisikiliza maelezo kutoka kwa mkandarasi  mshauri  msaidizi  kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara  katika kata ya Yombo Vituka.

Jengo la ghrorofa mbili linalojengwa katika zahanati ya Yombo vituka linavyoonekana kwa nje.

Kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es Salaam wakikagua  ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wasioona katika shule ya msingi Toangoma iliyopo kata ya Toangoma  Manispaa ya Temeke.


Kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es Salaam wakikagua  ujenzi wa vyoo katika shule ya msingi Toangoma iliyopo kata ya Toangoma  Manispaa ya Temeke.






..................HABARI KAMILI...............





Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam imekiri kufurahishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Temeke.Hayo yamesemwa  na Mwenyekiti wa kamati hiyo bibi Kate Silvia Kamba mara baada ya kumaliza ziara  jana majira ya saa 11 jioni.

Akizungumza baada ya kutembelea na kukagua miradi ya elimu,afya na barabara  bibi Kate  Kamba amesema ''Katika ziara yetu leo tumetembelea miradi mbalimbali,tumeona ujenzi wa kituo cha afya ambacho ni cha aina yake.tumeona ujenzi wa miundombinu ya maji, mabweni, madarasa, vyoo. Vilevile tumeona ujenzi wa barabara.Tulipita mwaka jana,lakini mwaka huu tumeona mambo makubwa,miradi imejengwa kwa viwango.Kwa kweli inafurahisha.Si hilo tu, tulipopita mwaka jana, kulikuwa na changamoto kubwa sana ya miundombinu,tulizamazama sana.Mwaka huu mambo ni tofauti,tumepita tunateleza  kwenye lami,lami imara ambayo tumeambiwa itachukua miaka 45.Hii inamaanisha kwamba ilani yetu haipo tu kwenye maandishi,bali ipo kwenye utekelezaji.Tuliyowaahidi wananchi tunayatekeleza kwa vitendo''.

Naye katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ndugu Zakaria Mwansasu  amewashukuru wananchi pamoja na watendaji wa manispaa. Hapa Mwansasu anasema''Tunawashukuru wananchi ambao ndio walipa kodi,kwani ndio waliotuwezesha, na sisi chama cha mapinduzi tuko hapa tunasimamia kuhakikisha kwamba kodi zao zinatumika sawasawa na jinsi ambavyo wametupa dhamana.Tunashukuru kwamba hata watendaji wetu wa halmashauri  ambao tumewapa dhamana ya kusimamia hayo,nao wanajitahidi sana kusimamia ,kwamba fedha zile ambazo zinatolewa,zinatumika ipasavyo.Kwa mara ya kwanza kuanzia tuanze kukagua miradi  hatujaona jengo lenye nyufa.Kwa mantiki hii 'ina maana kwamba force account' inatumika vizuri.Na ni kwa sababu linasimamiwa vizuri na watendaji.Ni jambo ambalo linafurahisha sana.Kituo hiki cha afya mpaka kitakapokamilika kitatumia sh.Bilioni 2 na milioni 125. Mpaka sasa imeshatumika sh. Bilioni 1 ,lakini kwa jinsi ilivyo ,unaona kabisa kwamba  fedha zilizotumika zimetumika sawasawa''.

Kamati ya siasa ya mkoa imetembelea miradi mbalimbali katika wilaya ya Temeke.Miradi hiyo ni ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kijichi iliyopo katika kata ya Kijichi,,Mradi wa ujenzi wa mabweni mawili ya wasioona na vyumba vitatu vya madarasa pamoja na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Toangoma,iliyopo katika kata ya Toangoma.Ujenzi wa shule ya msingi Marten Lumbanga iliyopo kata ya Kilungule. Ujenzi wa Zahanati ya Yombo vituka iliyopo katika kata ya Yombo Vituka.Mradi wa ujenzi wa barabara za 'Dar es Salaam Metropolitant Development Project' (DMDP) katika kata ya Yombo Vituka, pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji  katika kata ya Charambe.





..............MWISHO...............


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke