• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

KERO YA KUJAA MAJI SOKO LA VETENARI YATATULIWA

Posted on: January 27th, 2022

    

  Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Jokate Mwegelo siku ya  Januari 26, 2022 ameongozana na uongozi wa Machinga Taifa na Mkoa Dar es Salaam kufanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya visima, mitaro na makaro ya maji katika soko la Temeke Vetenari.

Katika ziara hiyo viongozi hao wameshuhudia namna  makaro na mifereji ya maji inavyosaidia Wafanyabiashara ndogondogo kwa kutatua kero ya kujaa maji katika maeneo hayo ya soko ambapo kabla ya ujenzi huo kulikuwa na adha kubwa ya kusimama kwa biashara kipindi cha mvua kutokana na kujaa maji mengi eneo hilo.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo Mkuu wa Wilaya amesema manispaa na Wilaya wameendelea kumuunga mkono  Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa vitendo kwa kutumia Shilingi 199,000,000 ya mapato ya ndani kujenga miundombinu hiyo ili kuboresha mazingira rafiki ya wafanyabiashara katika masoko.

"Niendelee kuwaahidi, kwa muongozo tuliopewa na Mhe. Rais, Mkuu wa Mkoa, katibu tawala Mkoa, kuwa tutaendelea kushirikiana katika kuboresha masoko na kutenga zaidi maeneo ya kuwapeleka Machinga wanapostahili wao kuwekwa". Alisema Mhe. Jokate

Sambamba na hayo Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa watendaji kutekeleza jukumu la kuhakikisha Machinga wanabaki katika maeneo waliopangiwa na kusimamia masoko kuhakikisha miundombinu hiyo inalindwa.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Machinga Taifa Ndugu Steven Lusinde na Mwenyekiti Mkoa Ndugu Yusuf Namoto wamesema leo wameamua kuungana na Mhe. Jokate kuweza kutekeleza agizo la Mhe. Rais juu ya uboreshaji wa miundombinu katika masoko ambapo wameonesha kufurahishwa na hali waliyoikuta soko la Vetenari huku wakiwataka Machinga kuendelea kutunza miundombinu hiyo na kuwataka  kubaki katika maeneo waliyohamishiwa.

Kadhalika, Wafanyabiashara wa soko hilo wamefurahishwa sana na ujenzi wa miundombinu hiyo kwa kuwasiaida sana kuondoa changamoto waliyokuwa wanakutana nayo kipindi cha mvua na uwepo wa makaro ya maji imekuwa suluhu kwa wauzaji vyakula (Mamalishe) kupata sehemu ya kumwagia maji machafu.

Ikumbukwe ujenzi huu wa miundombinu umetokana na kampeni ya uboreshaji wa mazingira ya ya Machinga katika masoko waliyohamishiwa kuendesha biashara zao.

Ikumbukwe ujenzi huu wa miundombinu umetokana na kampeni ya uboreshaji wa mazingira ya Machinga katika Masoko waliyohamishiwa kuendesha biashara zao mara baada ya kuhama kutoka barabarani ili kuwasaidia kurahisisha shuhuli zao za kila siku.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke