• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

KIGOMA YAWEKA KAMBI SIKU 3 KUJIFUNZA NAMNA TEMEKE INAVYOTEKELEZA UTOAJI WA MIKOPO YA 10%

Posted on: November 25th, 2020

Mkoa wa Kigoma kupitia wataalam wake umeweka kambi ya siku 3 kuanzia leo tarehe 25/11/2020 katika Manispaa ya Temeke kwa lengo la kujifunza namna Temeke ilivyofanikiwa kutekeleza agizo la Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe. Dkt John Pombe Magufuli katika utoaji wa mikopo ya 10% kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Wataalam hao wamezuru katika Manispaa ya Temeke wakiongozwa na kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt Vedast M. Makota ambaye anamwakilisha katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Ndg Rashid Mchata, viongozi wengine alioambatana nao ngazi ya Halmashauri ni Mkurugenzi wa Halmashari ya Kasuru,mwakilishi wa Mkurugrenzi Halmashauri ya Kibondo, vilevile Sekretarieti ya Mkoa  ambao ni Afisa biashara wa Mkoa, Afisa maendeleo wa Mkoa pamoja na baadhi ya wajasiriamali wa mkoa huo.

Akiongea wakati wa ziara ya kutembelea baadhi ya vikundi vya wajasiriamali ambao wamewezeshwa na Manispaa ya Temeke,Kaimu Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma amesema amevutiwa kuona viwanda vya kutengeneza bidhaa za Ngozi vikiendeshawa na vijana waliowezeshwa na Manispaa, viwanda vya ushonaji nguo, mradi wa usafishaji (usafi wa mazingira) ambao wamepatiwa gari kubwa la kuzolea taka ukisimamiwa na wanawake.

Vilevile kiwanda cha kusindika karanga mradi ambao unasimamiwa na wananawake wajasiriamali waliowezeshwa na Manispaa kupitia mikopo ya 10%.

Aidha kwa kuwa Serikali imekuwa ikitilia mkazo suala la kuwainua wananchi kiuchumi, na kwa upande wa mkoa wa Kigoma suala la mikopo ya 10% ni ajenda ya kudumu, sasa ziara yao katika Manispaa ya Temeke inakwenda kuboresha Mkoa na Wilaya zake namna bora na zenye tija za utoaji wa mikopo hiyo.

Amesema “Kigoma imeona umuhimu wa kuja Temeke kujifunza baada ya kufuatilia na kuona Manispaa ya Temeke inafanya vizuri katika kutoa mikopa ya 10% kwa wanawake,vijana na Watu wenye ulemavu.”

Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii na Vijana Manispaa ya Temeke Bi Herieth Makombe akifafanua utoaji wa mikopo ya 10% mbele ya wageni hao amesema Manispaa ya Temeke imekuwa ikitekeleza mikopo hiyo tofauti kidogo na Halmashauri zingine nchini. Temeke imekuwa ikitoa vifaa vya uzalishaji na sio pesa, pesa inatolewa kwa sehemu ndogo sana ambayo ni tsh 100,000/= hadi 2,000,000/= tu.

Aidha kupitia utaratibu huo unawawezesha wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kumiliki viwanda, kupata ajira na pia kurahisisha suala la marejesho kwa kuwa kama wanakikundi watashindwa kurejesha mikopo yao wananyang’anywa vifaa.

Sambamba na hilo Manispaa ya Temeke imejidhatiti kwa vitendo kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania za kufikia uchumi wa kati, ili kufikia uchumi huo lazima kuwekeza katika viwanda vikubwa, vya kati na vidogovidogo.




Baadhi ya matukio katika picha, wataalam kutoka Kigoma wakiwa katika miradi anuai inayotekelezwa Temeke.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke